Rais Samia aagiza Tume kuchunguza, kujua haki wanayoidai vijana

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Samia Suluhu Hassan ameielekeza Tume Huru ya Uchunguzi matukio yaliyotokea uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, kuchunguza sababu ya vijana walioingia barabarani siku hiyo kudai haki na  kujua ni haki gani wanadai ili waweze kuifanyia kazi wapate haki yao.

Akizungumza leo Novemba 20, 2025, Ikulu Chamwino, Dodoma, wakati wa uzinduzi wa tume hiyo, Rais Samia ameitaka Tume hiyo kutazama sura nzima ya mgogoro, ikiwemo mitazamo, matamko na hatua za wadau wote.

Aidha amesema Tume hiyo itachunguza matamshi ya viongozi wa vyama vya siasa kabla ya uchaguzi, uhusiano wao na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, pamoja na taarifa zinazoonyesha kuwa baadhi ya vijana walilipwa fedha kushiriki maandamano yaliyofanyika wakati huo.

“Jambo lile lilipotokea vijana waalingizwa barabarani kudai haki, tunataka kujua haki gani ambayo hawa vijana wameikosa na kwa umoja wao waliingia barabarani kudai haki hiyo. lengo la wale vijana kuingia barabarani ili tuweze kuifanyia kazi na wapate haki yao,

“Tunapokwenda kufanya hii kazi twende tukaangalie matamshi ya vyama vya upinzani wale waliokuwa wakisema lazima kiwake, hapakaliki, lazima aondoke, lazima kiwe hiki uchaguzi hautafanyika kitu gani hadi kilichowaletea kufanya vile lakini katika kufanya hivo tuangalie uhusiano wa hicho chama Tume yetu ya Uchaguzi, uhusiano wao ulikuwaje katika kipindi hicho mpaka ikawapelekea waseme maneno yale,” amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Ameeleza kuwa ana imani kubwa na Tume kutokana na sifa na ubobevu wa wajumbe wake katika kutimiza kazi ya uchunguzi wa kilichotokea hasa baada ya wapinzani kuonesha wasiwasi juu uwezo wa Tume hiyo ya ndani.

“Lakini niseme kwamba nina matumaini makubwa na tume hii, jana nilikuwa nasoma ‘article fulani wenzetu wapinzani wanasema hawana imani na Tume yoyote ya ndani wanataka Tume itoke UN, EU, AU ndio zije zifanye kazi hapa Tanzania. Lakini mimi nina imani kubwa na Tume hii,” amesema.

Amesema ni ni mzigo mkubwa wamepewa wajumbe wa Tume hiyo ya Uchunguzi, lakini kwa sifa zao anaamini wataweza.

Rais Dk. Samia aliunda Tume hiyo Novemba 18, 2025 kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Uchunguzi ya mwaka 2023(sura 32), Mwenyekiti wake akiwa ni Jaji Mstaafu, Mohamed Chande Othman na imepewa muda wa miezi mitatu.

Wajumbe wa Tume ni Jaji Mkuu Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Ibrahim Juma na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Balozi Radhia Msuya, Balozi Paul Meela na Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mstaafu (IGP) Said Mwema.

spot_img

Latest articles

DC Mpogolo: viongozi wa Serikali za Mitaa ni watu muhimu Katika Usimamizi wa Huduma za Umeme

Na Tatu Mohamed VIONGOZI wa Serikali za Mitaa wametajwa kuwa watu muhimu katika kusimamia miundo...

Bado denial inasuta nafsi za wengi, hatuwezi kupona

LEO ni siku ya 23 tangu risasi ya kwanza ilipofyatuliwa na kuua vijana waliokuwa...

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...

Yanga yatua Zanzibar kuitengenezea dozi AS FAR Rabat

Na Winfrida Mtoi Kikosi cha Yanga kimetua visiwani Zanzibar kwa maandalizi ya kuikabili AS FAR...

More like this

DC Mpogolo: viongozi wa Serikali za Mitaa ni watu muhimu Katika Usimamizi wa Huduma za Umeme

Na Tatu Mohamed VIONGOZI wa Serikali za Mitaa wametajwa kuwa watu muhimu katika kusimamia miundo...

Bado denial inasuta nafsi za wengi, hatuwezi kupona

LEO ni siku ya 23 tangu risasi ya kwanza ilipofyatuliwa na kuua vijana waliokuwa...

Watoto mapacha wajinyonga Zanzibar, kisa kazi za ndani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa...