Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la kujinyonga kwa watoto wawili wa kike wenye umri wa miaka 11, lilitokea katika Kijiji cha Kwale Mpona, Wilaya ya Wete, mkoani humo na kusema uchunguzi wa awali unaonesha sababu ni kukataa kufanya kazi za ndani walizoamrishwa na mama yao mzazi.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba,William Mwalliam Mwampaghale, tukio hilo limetokea Novemba 17, 2025 na miili ya watoto hao waolikuwa wanafunzi wa darasa la tano katika skuli ya Msingi Kizimbani, ilikutwa ikining’inia katika Kamba juu ya mti.
Amesema aliyegundua miili hiyo mita 100 kutoka nyumbani kwao, ni mama mzazi wa watoto hao, Sada Maohammed Omar baada ya kuanza kuwatafuta.
“Miili ya marehemu hao imefanyiwa uchunguzi na daktari wa hospitali ya Wilaya ya Wete iliyopo Kinyasini na kisha kukabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya tararibu za mazishi. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa sababu ya tukio hilo ni kukataa kufanya kazi za ndani walizoamrishwa na mama yao mzazi na kukimbilia nje na kwenda kusikojulikana ndipo miili yao ilipopatikana wakiwa washajinyonga,”amesema.



