Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2025 unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba, 2025 ni halali kwakuwa umefuata misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria za Uchaguzi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameyasema hayo katika Mkutano na Vyombo vya Habari uliofanyika Ofisini kwake Mtumba Jijini Dodoma, tarehe 28 Oktoba, 2025.

Akizungumza katika mkutano huo Mhe. Johari amesema kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni kwa mujibu wa masharti yaliyowekwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameeleza kuwa, ni haki ya kila Mtanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kama ilivyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Ibara ya 5(1) ya Katiba yetu inatoa haki kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka kumi na minane kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania na Wananchi.” Amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika hatua nyingine, Mwanasheria Mkuu wa Serikali amewakumbusha wananchi kuwa kutokana na masharti yaliyowekwa na wananchi katika katiba, Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, unafanyika kila baada ya miaka mitano kama ilivyoanishwa katika Ibara za 42(2) na 65(1) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kifungu cha 56(1) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024.

“Naomba mfikishe ujumbe kwa wananchi wote kuwa, miaka mitano imeshamalizika kwa mujibu wa Katiba na sasa uchaguzi wa kesho upo kwa mujibu wa Katiba hiyo na kwamba wagombea wote wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani nchi nzima wamepatikana kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo uchaguzi huu ni halali,” amesema Johari.

Vilevile, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ametumia Mkutano huo kutoa onyo kwa wote wanaopanga kuvuruga au kushawishi wananchi kutokushiriki uchaguzi ni kosa kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 129 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...