Elimu ya Nishati safi ya kupikia yawafikia maafisa dawati ngazi ya mikoa na Halmashauri

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia kwa Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati.

Akifungua mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vijiji.

Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kupikia katika ngazi ya taasisi, kaya n.k akitoa mfano kuwa asilimia 76 ya taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 mkoani humo zimeshahamia kwenye nishati safi ya kupikia.

Aidha, amewapongeza Watendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) ambao wanashirikiana na Mkoa wa Pwani kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ikiwemo utoaji mitungi ya gesi kwa bei ya ruzuku.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Nishati Safi ya Kupikia kutoka Wizara ya Nishati, Ngereja Mgejwa ameeleza kuwa mafunzo kuhusu Nishati Safi ya Kupikia yameanza kutolewa wilayani Kibaha, mkoani Pwani kwa kuhusisha Mikoa ya Pwani, Morogoro, Dar es Salaam, Mtwara, Lindi na Tanga.

Ameongeza kuwa, elimu ya nishati safi ya kupikia itaendelea kutolewa kwa Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia katika mikoa mingine iliyosalia kwani lengo ni kutoa elimu husika katika Mikoa yote 26 pamoja na Halmashauri zake.

Amesema kuwa suala la matumizi ya nishati safi ya kupikia ni kipaumbele cha nchi na dunia kwa ujumla ili kuondokana na athari zake katika mazingira, afya na kiuchumi.

Naye, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Wizara ya Nishati, Neema Mbuja ameeleza kuwa mafunzo yanayotolewa kwa maafisa dawati hao yanahusisha pia masuala ya Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia.

Ameeleza kuwa ili kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu nishati safi ya kupikia ni muhimu maafisa dawati hao wakafahamu njia za mawasiliano zitakazowasadia kufikisha elimu na jumbe zitakazotumika kuendana na maeneo wanayoyasimamia.

Ameongeza kuwa uwepo wa Mkakati wa Taifa wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia (National Clean Cooking Communication Strategy) unatoa mwongozo wa namna wadau watakavyoshirikiana kutoa elimu kwa umma ili kuondoa dhana potoshajii (misconception) kuhusu nishati safi ya kupikia na kubadili mitazamo hasi kuwa chanya kwa lengo la kuleta mabadiliko katika utekelezaji wa ajenda ya kitaifa ya nishati safi ya kupikia.

spot_img

Latest articles

Watumishi wa umma waaswa kushiriki Uchaguzi wa Oktoba 29

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imetoa wito kwa watumishi wote...

Jaji Mwambegele Akagua Maandalizi ya Vituo Maalum vya Kupigia Kura Wilayani Tanganyika

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa...

Simba nayo yaenda hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika

Na Winfrida Mtoi Mabao ya ugenini yameibeba Simba kwenda makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada...

Mrindoko: Mradi wa TACTIC utanufaisha wananchi wa Mpanda

Na Mwandishi wetu, Katavi MKUU wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amesema utekelezaji wa Mradi...

More like this

Watumishi wa umma waaswa kushiriki Uchaguzi wa Oktoba 29

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imetoa wito kwa watumishi wote...

Jaji Mwambegele Akagua Maandalizi ya Vituo Maalum vya Kupigia Kura Wilayani Tanganyika

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa...

Simba nayo yaenda hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika

Na Winfrida Mtoi Mabao ya ugenini yameibeba Simba kwenda makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baada...