Na Mwandishi Wetu
Treni ya Mwendokasi (SGR) imeacha njia yake na kupata ajali katika eneo la Ruvu Mkoani Pwani asubuhi ya leo Oktoba 23,2025 wakati ikitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Reli Tanzania, ajali hiyo imetokana na hitilafu za kiuendeshaji na hakuna kifo.
‘Timu ya wataalamu wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, uongozi wa TRC na vyombo vya ulinzi na usalama wamefika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa kina na juhudi za kuhakikisha kwamba huduma zetu zinarejea haraka,’ imesema taarifa hiyo.
