Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo Kuu la Songea, ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania (SAUT) – Mwanza, aliyeripotiwa kupotea mnamo Oktoba 09, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 17,2025  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Marco  Chilya, amesema Padre huyo hakutekwa kama ambavyo ilidhaniwa bali alijipoteza kutokana na sababu za msongo wa mawazo.

Kamanda huyo ameeleza kuwa Padre amepatikana akiwa hai katika mashamba ya Kijiji cha Mawa, kilichopo Kata ya Hanga, Wilaya ya Namtumbo ambapo ni nyumbani kwao.

Aidha ameongeza kuwa Padre huyo alikutwa akiwa  amedhoofika kwa njaa huku akiwa na begi dogo la mgongoni ambalo lilikuwa na taulo alilokuwa akitumia kulalia, hati yake ya kusafiria, karanga alizokuwa akitumia kama chakula, maji, funguo ya chumba alichokuwa akitumia kabla ya jimboni kwake, fedha taslimu kiasi cha Shilingi 13,500, saa ya mkononi, simu ya mkononi akiwa ameizima  pamoja na dawa za  maumivu.

Ameeleza kuwa  kwa sasa Padre huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songea (Homso) akiendelea na matibabu kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

spot_img

Latest articles

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Waangalizi wa Uchaguzi watakiwa kutoingilia mchakato wa Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAANGALIZI wa Uchaguzi wa ndani na wa kimataifa wametakiwa kuzingatia sheria...

Serikali yajipanga kuzalisha vijana wenye ujuzi na ubunifu kukidhi soko la ajira

Na Tatu Mohamed SERIKALI imesema itaendelea kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanapata elimu na mafunzo ya...

More like this