EWURA yatoa rai kuhusu vibali vya ujenzi wa Vituo vya Mafuta

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa rai kwa wafanyabiashara wanaokusudia kuanzisha vituo vya mafuta kuhakikisha wanapata kibali cha ujenzi kutoka EWURA kabla ya kuanza ujenzi.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 3 Oktoba 2025, mkoani Iringa na Meneja wa Kanda ya Kati wa EWURA, Hawa Lweno, wakati wa mkutano na wadau wa sekta ndogo za mafuta, umeme na maji.

Lweno amesema kumekuwa na mwitikio mkubwa wa wafanyabiashara kufungua vituo vya mafuta hasa maeneo ya vijijini, lakini changamoto imeibuka pale ambapo baadhi yao huanza ujenzi bila kuwa na kibali cha EWURA.

“Natoa wito kwa yeyote mwenye nia ya kuanzisha kituo cha mafuta kuhakikisha kwanza anapata kibali kutoka EWURA kabla ya kuanza ujenzi. Kukiuka sharti hili la kisheria kutasababisha mfanyabiashara husika kutozwa faini ya shilingi milioni 20,” amesema.

Kibali hicho ni muhimu kwa kuwa kinatoa nafasi kwa wataalamu wa EWURA kuhakiki na kujiridhisha kwamba ujenzi wa kituo husika unazingatia viwango na masharti ya kiafya, kiusalama na kimazingira yaliyowekwa.

Kwa upande wake, mmoja wa washiriki wa mkutano huo, David Mlyapatali, amesema kikao hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwani kimewapa uelewa zaidi kuhusu taratibu na wajibu wao katika kuendesha biashara hizo.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this