Na Mwandishi Wetu, The Media Brains
Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabosi wapya wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) maarufu Mwendokasi kwa kuwaondoa Mtendaji Mkuu Dk. Athuman Kihamia na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni UDART, Waziri Kindamba.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga, walioteuliwa ni Said Tunda anayechukua nafasi ya Dk. Kihamia na Pius Ng’ingo anayechukua nafasi ya Waziri Kindamba.
Uteuzi huo unakuja siku moja baada ya wananchi kufanya fujo kwa kupiga mawe mabasi hayo jana katika maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam kutokana na kuchoshwa na hali ya usafiri huo.
Wakati uteuzi huo unafanyika tayari mabasi mapya yameanza kufanya kazi katika njia ya Kimara, Gerezani, Kivukoni na Morocco.