Bei za Petroli, Dizeli zaendelea kushuka

Na Mwandishi Wetu

BEI ya mafuta ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Oktoba 2025 zimeendelea kushuka ambapo bei za rejareja za petroli zimepungua kwa sh. 55, dizeli sh 50 ikiwa ni muendelezo wa kupungua kwa bei za bidhaa hizo .

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Mwainyekule, kupungua kwa bei hizo kumetokana na kupungua kwa gharama za kubadilisha fedha za kigeni kwa wastani wa 5.10% huku gharama za kuagiza mafuta ya petroli kwa bandari ya Dar es Salaam zikipungua kwa wastani wa 1.95% .

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, imepungua kutoka sh 2,807 hadi 2,752 kwa petroli, na kutoka sh. 2,754 hadi sh. 2,704 kwa dizeli huku bei ya mafuta ya taa ikisalia kuwa sh. 2,774 kama ilivyokuwa Septemba 2025.

Mafuta ya petroli yaliyopokelewa katika Bandari ya Tanga, bei ya rejareja nayo imepungua kutoka sh. 2,868 hadi sh. 2,813, dizeli kutoka sh 2,816 hadi sh. 2, 766 na bei ya mafuta ya taa ikisalia kuwa sh. 2,835 kama ilivyokuwa kwa mwezi uliopita.

Kwa upande wa mafuta yanayopokelewa Bandari ya Mtwara, bei ya petroli imepungua kutoka sh. 2,899 hadi sh. 2,844, na dizeli kutoka Sh. 2,847 hadi 2,797 huku bei ya mafuta ya taa ikisalia sh 2, 866 kama ilivyokuwa Septemba 2025.

spot_img

Latest articles

TRA yakusanya Trilioni 8.97 kwa robo ya kwanza, yazidi lengo kwa asilimia 106.3

Na Mwandishi Wetu  MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza mafanikio ya makusanyo ya mapato kwa...

Rais Samia awapiga chini mabosi Mwendokasi

Na Mwandishi Wetu, The Media Brains Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa mabosi wapya...

Kiti Baraza la Usalama kitaondoa maafa Afrika?

MKUTANO Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa wa 80 ulimalizika jijini New York,...

Jamii yatakiwa kupaza sauti kukomesha ukatili wa kijinsia

Na Tatu Mohamed JAMII imetakiwa kuendelea kupaza sauti kwa pamoja ili kutokomeza ukatili wa kijinsia...

More like this