THBUB yawaasa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu

TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), imewaasa waandishi wa habari nchini, kujiepusha kuchapisha, kutangaza habari zenye lengo la kuchochea vurugu, ubaguzi, chuki za kisiasa, kikabila, kidini na jinsi.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa THBUB, Patience Ntwina,, wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo Jumatatu Septemba 22, 2025 katika Ukumbi wa Tume hiyo, Luthul, Dar es Salaam.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa kuhusu Haki za Binadamu na Wajibu wa Waandishi wa Habari wakati wa uchaguzi, Ntwina, alisema kipindi cha kupiga kura katika Uchaguzi MKuu wa Urais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, mwaka huu, waandishi wa habari wanatakiwa kuepuka kufanya kampeni kwa namna yoyote.

Nkwina alisema siku ya kupiga kura haitakiwi kuvaa mavazi yenye alama ya chama au mgombea fulani. Ametoa with kwa waandishi wa habari kuchukua tahadhari dhidi ya matumizi ya mabaya ya majukwaa ya habari ikiwamo mitandao ya kijamii.

Pia amevitaka vyombo vya habari kujikita katika kuimarisha amani, utulivu na demokrasia nchini kwa kutotumika vibaya kalamu zao.

spot_img

Latest articles

Simbu afichua siri ya ushindi

Na Winfrida Mtoi Bingwa wa Dunia wa mbio za Marathoni za kilomita 42, ambaye ni...

Baraza ataja mbinu za kuimaliza Yanga

Na Winfrida Mtoi Kocha Mkuu wa timu ya Pamba Jiji, Francis Baraza amesema hana presha...

Kocha Simba aaga, atangazwa Raja Casablanca

Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameaga rasmi wadau na mashabiki...

TARURA kushirikiana na Kampuni ya Sukari Kilombero kufanya matengenezo ya Barabara

Na Mwandishi Wetu WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kushirikiana na...

More like this

Simbu afichua siri ya ushindi

Na Winfrida Mtoi Bingwa wa Dunia wa mbio za Marathoni za kilomita 42, ambaye ni...

Baraza ataja mbinu za kuimaliza Yanga

Na Winfrida Mtoi Kocha Mkuu wa timu ya Pamba Jiji, Francis Baraza amesema hana presha...

Kocha Simba aaga, atangazwa Raja Casablanca

Na Mwandishi Wetu Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Fadlu Davids ameaga rasmi wadau na mashabiki...