Mvua za vuli kunyesha kwa wastani  kuanzia  Oktoba

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa msimu wa mvua za vuli kwa mwaka 2025, unaotarajiwa kuanzia Oktoba hadi Desemba, utakuwa na mvua za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya nchi.

Msimu huo utatawaliwa na vipindi virefu vya ukavu pamoja na mtawanyiko usioridhisha wa mvua, hasa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk. Ladislaus Chang’a, wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Oktoba 2025 katika maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Amesema kuwa mvua hizo zitaendelea kusambaa katika maeneo ya Pwani ya Kaskazini na Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki kuanzia wiki ya kwanza hadi ya pili ya mwezi Novemba 2025.

“Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari 2026, mvua za vuli zinatarajiwa kuongezeka kidogo mwezi Desemba 2025, huku vipindi vya joto kali kuliko kawaida vikitarajiwa kutokea katika msimu huo”Amesema Chang’a

Aidha Dk. Chang’a ametoa wito kwa wananchi kufuatilia kwa karibu taarifa mbalimbali za hali ya hewa zinazotolewa na TMA, zikiwemo utabiri wa saa 24, siku 10, na mwezi mmoja, pamoja na tahadhari zinazotolewa mara kwa mara.

Ameeleza kuwa mwelekeo huo wa msimu ni wa muda wa miezi mitatu, hivyo mabadiliko ya muda mfupi na mwenendo wa mifumo ya mvua yataendelea kufuatiliwa na kuwasilishwa kwa wakati.

spot_img

Latest articles

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

Viongozi wa dini waendelea kihimiza amani uchaguzi mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam VIONGOZI wa dini nchini wameendelea kuhimiza umuhimu wa kudumisha...

Ujumbe wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 katika Kongamano la Kamati ya Amani Kitaifa Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu Askofu Mkuu Wapo Mission, Dk. Sylvester Gamanywa “Mungu ambaye tunamwakilisha ndiye anayweka watawala...

Watumishi wa umma waaswa kushiriki Uchaguzi wa Oktoba 29

Dar es Salaam. Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) imetoa wito kwa watumishi wote...

More like this