Ajali yaua wanafunzi wawili wa kidato cha sita

Na Mwandishi Wetu

Watu saba wamefariki dunia wakiwamo wanafunzi wawili wa kidato cha sita shule ya Sekondari Songe, Musoma baada ya gari aina ya Toyota Succeed walilokuwa wakisafiria kugonga kwa nyuma Fuso lililokuwa limeegeshwa barabarani baada ya kuharibika.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Mark Njera, ajali hiyo imetokea Kijiji cha Buganjo wilayani Rorya leo Septemba 11,2025 saa 11 alfajiri.

Amewataja wanafunzi hao kuwa ni Kwinta Gerald(18) Anitha Selemani(18). Wengine waliofariki ni Kelivin Orando(28), Ombura Ududo(34), John Abraham(30), Sharome Benard(30) wote wakazi wa Rorya.

Kamanda Njera amesema uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali hiyo ni  ni mwendokasi wa dereva wa gari aina ya Toyota Succeed kwa kuendesha bila kuchukua tahadhari.

Ameeleza kuwa dereva wa gari aina ya Mitsubish Fuso iliyokuwa  imeharibika na kupaki pembeni  mwa barabara ilichukua tahadhari  kwa kuweka  alama(reflective triangle).

spot_img

Latest articles

Mvua za vuli kunyesha kwa wastani  kuanzia  Oktoba

Na Mwandishi Wetu Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetangaza kuwa msimu wa mvua...

Tembo Warriors yatinga nusu fainali CECAAF

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya watu wenye ulemavu Tanzania 'Tembo Warriors' imefanikiwa kutinga...

Mpina ashinda kesi, ruksa kugombea Urais

Na Mwandishi Wetu Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina leo Septemba...

Mahakama kuamua hatma ya Lissu Jumatatu

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Tundu Lissu,  amerejeshwa...

More like this