DC Msando aridhishwa uzalishaji maji Ruvu, atoa maagizo Dawasa

Na Mwandishi Wetu

MKUU cmwa Wilaya ya Ubungo (DC), Albert Msando amefanya ziara katika mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu kwa lengo la kuona na kujiridhisha hali ya uzalishaji wa maji katika mtambo huo ambao unahudumia sehemu kubwa ya Wilaya ya Ubungo.

Katika ziara yake hiyo aliyoambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Ubungo pamoja na watendaji wa Dawasa, DC Msando ameridhishwa na hali ya uzalishaji maji huku akitoa maagizo kwa DAWASA kutatua changamoto zilizopo kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji.

“Tumefika hapa Ruvu Juu na tumejiridhisha uzalishaji wa maji upo vizuri, tunafahamu kulikuwa na matengenezo yanaendelea na kusababisha baadhi ya maeneo kukosa maji tumeona matengenezo yamekamilika na huduma inarejea kwa wananchi,” amesema Msando.

Msando ametoa maagizo kwa watendaji wa DAWASA hasa waliopo Wilaya ya Ubungo kuhakikisha maji yanayozalishwa yanawafikia wananchi bila kikwazo na kutoa taarifa kwa wakati pale panapotokea changamoto yeyote ya huduma lakini zaidi wanaopata maji kwa migao wajue siku gani wanapata na ratiba hiyo isimamiwe bila kupindishwa.

“Nirudie kusema tena, swala la upotevu wa maji halikubaliki, Serikali inatumia gharama kubwa kuchakata maji haya mpaka yanapomfikia mteja uwekezaji huu lazima uthaminiwe na tusimamie vyema kila mwananchi apate maji,” amesema Msando.

Meneja wa Mtambo wa uzalishaji maji Ruvu Juu, Mhandisi Juma Kasekwa amesema kwasasa hali ya uzalishaji imerejea katika hali ya kawaida na maeneo yaliyokuwa hayapati maji, huduma inaendelea kuimarika.

“Katika hali ya kuboresha uzalishaji maji katika mtambo wetu wa Ruvu Juu, Serikali imetupatia zaidi ya Shilingi bilioni 1 kununua pampu mbili mpya ambazo ni mategemeo yetu mpaka ifikapo mwezi Novemba tutakua tumezifunga na Kuongeza uzalishaji wa maji,” amesema Kasekwa.

spot_img

Latest articles

Mo ajiondoa Bodi ya Wakurugenzi Simba,  Barbara Gonzalez arejea

Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, ametangaza  kuachana...

Ninatamani Tume ya Charles Keenja irudi Dar es Salaam

TAIFA lipo katika kampeni za uchaguzi mkuu ambao ni mahususi kusaka madaraka ya dola....

Serikali yaondoa pingamizi shauri la Mpina, kesi kusikilizwa Jumatatu

Na Mwandishi Wetu MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma imepanga kusikiliza kesi ya ACT...

Matumizi ya Nishati Safi kupikia yapata msukumo mpya

Na Mwandishi Wetu, Mwanza MATUMIZI ya nishati safi ya kupikia yamepata msukumo mpya jijini Mwanza...

More like this