Na Mwandishi Wetu
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma imepanga kusikiliza kesi ya ACT Wazalendo na Luhanga Mpina dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jumatatu Septemba 8,2025.
Shauri hilo limesikilizwa leo Septemba 3,2025 kwa njia ya mtandao mbele ya jopo la Majaji watatu, Jaji Evaristo Longopa, Jaji John Kahyoza na Jaji Abdi Kagomba ambapo Mahakama imeridhia kesi hiyo isikilizwe ndani ya siku tano kwa njia ya maandishi , huku Mawakili wa pande zote mbili wakitarajiwa takutana Mahakamani kufanya mjumuisho wa hoja zilizowasilishwa kwa maandishi mahakamani hapo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa ACT Wazalendo, upande wa Serikali umeamua kuondoa mapingamizi waliyokuwa wameweka awali kuhusiana na kesi hiyo, hatua ambayo imeongeza urahisishaji wa kusikiliza kesi ya msingi.
Kesi hiyo namba 21692/2025, iliyofunguliwa na Bodi ya Wadhamini wa ACT Wazalendo pamoja na Lugaha Mpina, ikipinga uamuzi wa INEC kumuengua mgombea wao wa Urais, katika orodha ya wagombea.
