Sungusungu kwenda jela miaka 60 kwa kumpa mimba mwanafunzi

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam imemhukumu Faridi Mohamedi maarufu  Sungusungu  kifungo cha miaka 60 jela, kuchapwa viboko sita na kumlipa mwathirika fidia kiasi cha sh  2,000,000 baada ya kupatikana na hatia ya makosa mawili,  kubaka na kumpa mimba mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye umri wa miaka 14.

Hukumu hiyo imetolewa Agosti 19, 2025 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, John Ngeka baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Awali imeelezwa mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo April 20,2024 maeneo ya Tandika Manispaa ya Temeke, baada ya kumlaghai mwanafunzi wakati akiwa njiani kuelekea shule na kumjengea mazoea ya kumpatia zawadi mbalimbali na baadae kufanikiwa kumpeleka nyumbani kwake na kumbaka na kisha kumpa ujauzito

Katika kesi hiyo ya Jinai namba 20311/2024 mtuhumiwa alishitakiwa kwa makosa mawili ya kubaka na kumpa mwanafunzi mimba.

Katika hatua nyinginye Mahakama ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara imetoa hukumu ya kifungo cha maisha jela kwa mshtakiwa Saidi Haruvi, mkazi wa Kijiji cha Engusero Wilayani Kiteto baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka tisa  ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi

Awali imeelezwa Mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo April 09, 2025 huko katika kijiji cha Engusero, Kiteto.

Akisoma hukumu hiyo Agosti 18, 2025 Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Kiteto, Boniphace Lyamwike ameeleza kuwa Mahakama imeridhishwa na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo ambao umemuunganisha mtuhumiwa kutenda kosa hilo na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

spot_img

Latest articles

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

Hizi ndizo hisia dhidi ya INEC, Msajili wa Vyama vya Siasa

KATIKA safu hii wiki iliyopita niliandika uchambuzi nikihoji, ‘INEC, Msajili wa Vyama wanaweza kutupa...

Mradi wa TACTICS waleta mageuzi ya miundombinu Morogoro

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuboresha miundombinu...

Geofrey Timothy achukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Kawe

Na Mwandishi Wetu MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Geofrey...

More like this