Prof. Kabudi: Uandishi wa Habari ni taaluma, anayefanya kazi hii lazima wawe na vigezo

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi amesema uandishi wa Habari na utangazaji ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine nchini akisisitza kuwa mtu yeyote anayetaka kutekeleza majukumu yanayohusiana na tasnia hiyo nchini Tanzania, lazima awe na elimu na vigezo vinavyotakiwa.

Prof. Kabudi amesema hayo Agosti 18, 2025 Jijini Mbeya alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa Mkutano wa wadau wa Habari na Utangazaji kutoka Mikoa ya nyanda za juu kusini wa kujenga uelewa wa pamoja kwa pande zote ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.

“Nalisema hili kwa uchungu sana, watu waliamini kuwa kuwa mwandishi wa Habari au mtangazaji ni kipaji na sio taaluma jambo ambalo sio kweli, uandishi wa Habari ni taaluma ambayo ina vigezo vya kufuata na maadili ya kuzingatia. Uandishi wa Habari ni taaluma nzuri, ni lazima tuijali” amesema Pro. Kabudi.

Ametoa wito kwa waandishi wa habari ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu ya kihabari bila kuwa na vigezo vya kitaaluma wajiendeleze ili waweze kupata ithibati akibainisha kuwa Serikali imeanzisha Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ili kulinda taaluma ya habari ambapo bodi hiyo imeingia makubaliano na vyuo vinavyotoa taaluma ya habari kikiwemo Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) ili kuwezesha wanahabari kusoma.

Katika hatua nyingine Waziri Kabudi ametoa wito kwa waandishi wa habari wazingatie weledi na kuwa wazalendo kwa nchi kutokana na umuhimu wao katika kulinda na kuhamasisha wananchi kuilinda na kuitetea na kuipenda nchi.

“Mwandishi wa habari unapokuwa mzalendo kwa kuipenda, kuienzi na kuithamini nchi yako haimaniishi kwamba haina changamoto na haina maana kuwa ndani ya nchi hakuna yaliyopungua la hasha ni kwa sababu unajua hiyo ndiyo nchi yako, mahali ulipozaliwa na mahali unapoishi” amesisitiza.

Amewataka waandishi wa habari waendelee kuzingatia taaluma kwa kuwa yapo mataifa ambayo chaguzi zao huishia kwenye machafuko kutokana na wagombea wao kuamua kujitangazia matokeo ya uchaguzi nje ya utaratibu wa taasisi rasmi zilizowekwa kisheria kutangaza matokeo jambo ambalo limekuwa chanzo cha kuvuruga amani.

spot_img

Latest articles

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

Serikali yaahidi kuimarisha uwezeshaji wa Makundi Maalum kupitia ajenda ya Maendeleo Jumuishi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt....

More like this

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...