Wananchi Manispaa ya Kigoma Ujiji waanza kunufaika na Mradi wa Tactic

Na Mwandishi Wetu, Kigoma

WANANCHI katika Manispaa ya Kigoma Ujiji wameanza kunufaika na mradi wa TACTIC unaotekelezwa chini ya Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa mkopo nafuu kutoka Benki ya Dunia.

Akielezea mradi huo unavyotekelezwa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji , Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Kisena Mabuba amesema kuwa mradi huo umejikita katika uboreshaji wa miundombinu ambapo kwa Manispaa hiyo kazi zinazofanyika ni pamoja na ujenzi wa mitaro ya maji, ujenzi wa daraja, masoko na barabara.

Aidha, ameongeza kuwa miundombinu hiyo inayojengwa inalenga kukuza uchumi wa wananchi na kuondoa kero za usafiri na usafirishaji huku akibainisha kuwa kipindi cha masika wananchi walikua wanapata shida kwani maji yaliingia katika makazi yao lakini kupitia mradi wa TACTIC tayari mitaro imejengwa na maji yanaelekezwa moja kwa moja ziwani.

“Kupitia mradi huu, tutapata barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 9.5 ambazo zitaunganisha Kata sita za Manispaa yetu, uwepo wa taa za barabarani pia utapendezesha Mji wetu,” amesema .

Kwa upande wake Mhandisi Julius Samwel ambaye ni mratibu wa mradi wa TACTIC ngazi ya Manispaa amesema kuwa miradi yote imeanza na utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali.

Wakiongea kuhusu miradi hiyo wananchi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wameonesha furaha yao juu ya utatuzi wa kero ya muda mrefu.

Mariam Athumani ambaye ni Mkazi wa Kigoma Ujiji amesema kuwa kabla ya ujenzi wa mifereji ,maji yaliingia katika makazi na kusababisha kero na uharibifu wa mali lakini kwa sasa yameelekezwa moja kwa moja ziwani.

Akiongea kuhusu ujenzi wa Soko la Mwanga, Hussein Hamis ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Kigoma amesema kuwa kukamilika kwa soko hilo kutachochea uchumi wa Mkoa kwani watapata wageni mbalimbali kutoka nchi za jirani zikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi ambao watafika kufanya biashara.

Kuhusu ujenzi wa Soko la samaki Katonga, wafanyabiashara wameipongeza Serikali kuleta mradi huo utakaowawezesha kufanya biashara kwa njia za kisasa na kukuza uchumi .

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...