Njiwa wa Mapambo wanaouzwa kwa Laki nne hadi milioni moja, wageuka kivutio Nanenane

Na Tatu Mohamed

NJIWA wa mapambo waliowasilishwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima na Wafugaji (Nanenane) yanayoendelea jijini Dodoma wamegeuka kivutio kikubwa kwa wananchi kutokana na muonekano wao wa kipekee pamoja na bei yao.

Mfugaji wa njiwa hao, Abdulaziz Almasi, amesema ameleta aina 10 tofauti za njiwa wa mapambo, ambapo kila mmoja huuza kuanzia shilingi laki nne (400,000) hadi kufikia milioni moja (1,000,000).

“Watu wengi wanashangazwa na bei, lakini hizi ni aina za kipekee za njiwa wa mapambo. Wengine wanatoka Marekani na Ujerumani. Muonekano wao, umbile na asili yao ndio vinawafanya kuwa wa gharama,” amesema Almasi.

Ameeleza kuwa njiwa hao wanaweza kufugwa kwa malengo ya mapambo au kibiashara, na kwamba hula mtama, choloko na uwele, huku wakizaliana kwa wingi.Almasi ambaye amejikita kwenye biashara hiyo kwa zaidi ya miaka 15, amesema alianza na njiwa sita tu, lakini hadi sasa anamiliki zaidi ya njiwa 2000 wa mapambo huku wakiwa wa aina zaidi ya 90.

Kwa mujibu wa Almasi, biashara hiyo ni fursa ambayo Watanzania wengi bado hawajaichangamkia kikamilifu, licha ya kuwa na soko la uhakika na faida kubwa endapo mfugaji atazingatia ubora na soko sahihi.

Banda lake limekuwa moja ya maeneo yanayovutia watu wengi kwenye maonesho hayo, ambapo baadhi ya waliotembelea wameonekana kushangazwa na uwepo wa njiwa wenye thamani inayofikia hadi milioni moja kwa mmoja.

Maonesho ya Nanenane mwaka huu yameendelea kuonyesha ubunifu wa sekta ya kilimo na mifugo, huku biashara ya njiwa wa mapambo ikiwa miongoni mwa maeneo yanayoibua mjadala mpya kuhusu kilimo mseto na uwekezaji wa aina tofauti vijijini na mijini.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this