Wizara ya Katiba na Sheria yasaidia kupunguza migogoro ya ardhi Nanenane

Na Tatu Mohamed

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Jabiri Shekimweri, amesema kuwa ushiriki wa Wizara ya Katiba na Sheria katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) yanayoendelea jijini Dodoma ni fursa muhimu ya kupunguza migogoro mbalimbali, hasa ya ardhi, ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza Agosti 6, 2025, mara baada ya kutembelea banda la wizara hiyo, Shekimweri alisema kuwa huduma zinazotolewa kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia zina umuhimu mkubwa kwa jamii, ikizingatiwa kuwa bado kuna malalamiko mengi yanayohusiana na masuala ya ardhi.

“Nimefurahi sana kukuta banda la Wizara ya Katiba na Sheria linatoa huduma hii ya msaada wa kisheria lakini pia linatoa elimu. Natoa wito kwa wananchi wote wafike hapa kupata huduma na elimu ya utatuzi wa migogoro, hasa wanawake wajitokeze kwa wingi kujifunza masuala ya mirathi kwani mara nyingi wao ndio wahanga wakuu,” amesema DC Shekimweri.

Ameongeza Wizara hiyo si tu inasikiliza na kushughulikia malalamiko ya wananchi, bali pia inawapa maarifa ya haki na wajibu wao kisheria, jambo litakalosaidia kuimarisha ustawi wa jamii na mshikamano.Shekimweri pia amepongeza elimu ya Haki na Utawala Bora inayotolewa na wizara hiyo kwa wananchi, akisema ni jambo muhimu kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.

“Tunaelekea katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, hivyo elimu ya haki, wajibu na utawala bora ni muhimu kwa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu na kwa uelewa mpana katika mchakato huo wa kidemokrasia,” amesisitiza.

Wizara ya Katiba na Sheria ni miongoni mwa taasisi zinazoshiriki kikamilifu katika Maonesho ya Nanenane kwa kutoa huduma za kisheria, elimu na ushauri kwa wananchi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali kupeleka huduma karibu na wananchi.

spot_img

Latest articles

Jeuri ya ushindi CAFCL Simba waanza ‘kuchonga’

Na Winfrida Mtoi Ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika mchezo wa Ligi ya...

Viongozi wa dini wahimiza Watanzania kupiga kura, amani

Na Mwandishi Wetu, Mwanza VIONGOZI wa dini mbalimbali mkoani Mwanza, wametoa wito kwa Watanzania kujitokeza...

Chalamila amkabidhi mjane Alice Haule Hati ya Nyumba

Na Tatu Mohamed MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemkabidhi hati ya...

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

More like this