Wizara ya Nishati na Taasisi zake zashiriki maonesho ya kimataifa ya Kilimo Dodoma

Na Mwandishi Wetu

WIZARA ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake zinashiriki katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ambayo yameanza Agosti 1 katika Viwanja Nzuguni Jijini Dodoma.

Maonesho hayo yamebebwa na kaulimbiu ya ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi 2025’.

Katika maonesho hayo ambayo yamefunguliwa na Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, Watalaam wa Wizara pamoja na kueleza mafanikio yaliyofikiwa katika Sekta ya Nishati ikiwemo ukamilishaji wa Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere na Usambazaji wa Umeme Vijijini, wanatoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia.

Aidha wananchi wanafahamishwa kuhusu mipango mbalimbali ambayo Wizara imepanga kutekeleza katika mwaka wa fedha 2025/2026 ikiwemo kuendelea kusambaza umeme vitongojini na utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia.

Taasisi za Wizara ya Nishati zinazoshiriki maonesho hayo ni Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania ( TPDC), Wakala wa Nishati Vijijini ( REA) Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA) na Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania ( TGDC).

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this