Katibu Mkuu Kiongozi kufungua mafunzo kwa watendaji wakuu taasisi za umma

Na mwandishi wa OMH, HDar es Salaam

KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo ya siku nne kwa watendaji wakuu wa taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali.

Mafunzo hayo yatakayofanyika kuanzia Julai 28-31, 2025 katika shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere, Kibaha, mkoani Pwani, yanaratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Taasisi ya Uongozi.

Lengo la mafunzo hayo kwa watendaji wakuu wapya na wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo ni kuwajengea uwezo watendaji wakuu ili watekeleze majukumu yao kwa weledi na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu Alhamisi, Julai 24, 2025, alisema Program ya mafunzo kwa watendaji wakuu ni kielelezo dhahiri cha dhamira ya dhati ya serikali ya awamu ya sita ya kuhakikisha kuwa watendaji wanajua nini wanatakiwa kwenda kufanya katika taasisi walizopewa kuongoza.

“Mafunzo haya yanayolenga kuongeza tija na ufanisi katika taasisi za umma, ni endelevu,” alisema Mchechu.

Ikumbukwe kwa mara ya kwanza mafunzo haya yalifanyika Oktoba 2024, Mchechu alisema kuwa programu hiyo ya mafunzo ni mwendelezo wa hatua mbalimbali ambazo Ofisi ya Msajili wa Hazina inachukua katika kutafsiri na kutekeleza kwa vitendo maono ya Mheshimwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na falsafa ya 4Rs.

“Katika falsafa ya 4Rs tumejikita katika R mbili kati ya nne ambazo ni Reform (mabadiliko) na Rebuild (kujenga upya),” alisema.

Alifafanua: ”Hapa tutajikita zaidi katika eneo la kuwajengea uwezo watendaji wakuu ili wawe na ufanisi zaidi katika usimamizi wa taasisi za umma.”

Ofisi ya Msajili wa Hazina inasimamia jumla ya taasisi, mashirika ya umma, wakala wa serikali na kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache 308, huku uwekezaji ukiwa n Sh86.25 trilioni.

Kati ya kiasi hicho Sh83.33 trilioni zimewekezwa kwenye taasisi, mashirika ya umma na wakala wa serikali, huku Sh2.92 trilioni zikiwekezwa kwenye kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...