FCC yawahamasisha wananchi kulinda Afya na Haki zao dhidi ya Bidhaa Bandia

Na Tatu Mohamed

TUME ya Ushindani (FCC) imewataka wananchi kuwa mstari wa mbele katika kulinda afya na usalama wao kwa kujiepusha na bidhaa bandia, huku ikisisitiza umuhimu wa elimu kwa jamii kuhusu haki za walaji na mazingira salama ya biashara.

Kauli hiyo ilitolewa Julai 4, 2025 na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Hadija Ngasongwa, alipotembelea Banda la Viwanda na Biashara katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

“FCC haishughulikii tu makampuni au wawekezaji, bali inalinda afya ya jamii nzima. Tuna jukumu la kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa salama, bora na zinazokidhi viwango vya kisheria,” alisema Hadija.

Alibainisha kuwa moja ya changamoto kubwa kwa jamii ni upatikanaji wa bidhaa bandia, ambazo zinaweza kuleta madhara ya kiafya, kiuchumi na kijamii.

“Elimu ni silaha kuu. Tunawahimiza wananchi kufika kwenye banda letu kujifunza namna ya kuzitambua bidhaa bandia,” aliongeza.

Hadija alisema FCC imekuwa ikitoa elimu kwa walaji kuhusu haki zao, ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi ya manunuzi, kudai stakabadhi, na kuripoti bidhaa zisizo salama.

Pia aliwahamasisha wananchi wa kipato cha chini kuchangamkia fursa zinazopatikana kupitia maonyesho ya Sabasaba kwa kushirikiana na kampuni mbalimbali ili kukuza biashara zao kwa njia halali.

“Tunataka jamii ielewe kuwa kulinda haki ya mteja ni kulinda jamii nzima. Ndiyo maana tumeleta wataalamu wetu kutoa elimu moja kwa moja hapa Sabasaba,” alisema.

Kwa ujumla, FCC inatumia jukwaa la Sabasaba sio tu kusimamia ushindani wa haki, bali kama daraja la kuunganisha elimu, usalama wa jamii na kukuza mazingira bora ya biashara kwa Watanzania wote.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...