Rais Mwinyi awatunuku Kamisheni Maafisa wapya wa Idara  Maalum za SMZ

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewatunuku Kamisheni Maafisa wapya 164 Mkupuo wa 06 kwa mwaka 2024-2025 wa Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza na Maafisa hao wakati wa hafla ya kufunga kozi hiyo, amewasisitiza kuyatumia mafunzo na elimu waliyoipata ili kuleta mabadiliko chanya na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo ya kazi.

Hafla hiyo imefanyika leo Juni 26, 2025 katika Chuo cha Uongozi cha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Dunga, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo Maafisa hao ni kutoka Jeshi la Kujenga Uchumi na Kikosi cha Valantia.

Aidha Rais Mwinyi amesema kuwa Serikali inaendelea kuziamini Idara Maalum za SMZ kwa ajili ya ulinzi wa nchi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo itaendelea kuimarisha maslahi ya wapiganaji hao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi na bidii kwa lengo la kuchangia maendeleo ya nchi.

Halikadhalika, amewasisitiza Maafisa hao kudhihirisha elimu na mafunzo waliyoyapata kwa vitendo ili kuleta mabadiliko chanya, kuongeza ufanisi, na kuzingatia sheria na miongozo ya kudumu ya Idara za SMZ.

Amesema kuwa Serikali inakusudia kukifanya chuo hicho kuwa cha kimataifa na kitovu cha kuandaa Maafisa wa Idara Maalum za SMZ wenye weledi na uadilifu.

Kwa upande mwingine, Rais  Mwinyi pia amelipongeza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ushirikiano wake katika kufanikisha mafunzo ya Maofisa hao, na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano huo wakati wote.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this