Wanaume wana haki ya kulindwa- IGP Wambura

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amesema wanaume nchini wana haki ya kulindwa, kusikilizwa na kupewa heshima ambapo wametakiwa kutumia ofisi za Dawati la Jinsia kuripoti ukatili wanaofanyiwa majumbani.

IGP Wambura amesema hayo wakati akifungua Mradi wa Jengo la ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Tarime, Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya ambapo jengo pamoja na samani zake limegharimu kiasi cha Sh 300 milioni  ikiwa ni  ufadhiri serikali ya Finland.

Aidha, IGP Wambura amewakumbusha wananchi kuwa, serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali imeweza kuweka mikakati madhubuti katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ikiwemo makosa ya ukeketaji ili kuhakikisha kuwa wanaojihusisha na vitendo hivyo wanadhibitiwa kwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia watendaji wa dawati hilo la jinsia wametakiwa kuhakikisha kuwa, wanatoa huduma zenye viwango kwa wateja au wahanga wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na kutafuta ufumbuzi wa kukomesha vitendo vya ukatili kwenye jamii.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this