GFA yaweka rekodi uundaji magari nchini, yakamilisha gari ya 4000

Na Mwandishi Wetu

Kiwanda cha kwanza kutengeneza na kuunganisha magari Tanzania cha GF Vehicles Assemblers (GFA), kilichopo Kibaha mkoani Pwani, kimeweka rekodi ya uundaji magari baada ya kusheherekea kufikia utengenezaji wa idadi ya magari 4000 tangu kilipoanza uzalishaji rasmi wa magari mwaka 2020.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 4000 kukanyaga aridhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kutembea ,Meneja mkuu wa kiwanda hicho ,Ezra Mereng amesema wanaishukuru Serikali kupendekeza tozo ya maendeleo ya viwanda kwenye vichwa vya Terla za magari makubwa vinavyoagizwa nchini kwa asilimia 10 ili kuvilinda viwanda vya ndani na kuchochea ununuzi wa magari yalionunganishwa nchini.

Mkurugenzi wa GF Vehicles Assemblers (GFA), Ally Karmali akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa sherehe za uundwaji wa gari ya 4000 iliyotengenezwa katika kiwanda hicho na mafundi wa ndani kutoka vyuo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wataalamu wa kigeni iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa GFA, All Jawad Karmali amesema wamejipanga kuhakikisha wanaongeza mtaji katika uwekezaji ili kukabiliana na soko la Afrika mashariki na kati kwa upande wa magari.

Ameeleza kuwa wanataka kuifanya Tanzania kuwa nchi moja wapo inayounganisha magari na kulisha ukanda wote wa Afrika Mashariki kutokana na mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyotengenezwa na Serikali.

Pia alizitaka tasisisi za serikali na kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa ili kazi ya kuunganisha ifanyike na viwanda vya ndani kwa lengo la kukuza pato la Taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, pia nchi kujipatia fedha za kigeni kwa kuuza magari yanayotoka Tanzania kwa nchi jirani.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...