Chodawu yawakumbuka watoto wachanga Hospitali ya Amana

Na Mwandishi wetu

CHAMA cha Wafanyakazi Majumbani (CHODAWU), kimeungana na watu mbalimbali duniani kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani ambayo huadhimisha Juni 16, kila mwaka.

Chodawu katika kuadhimisha siku hiyo kimetembelea Hospitali ya Amana katika wodi ya watoto wachanga na kutoa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia watoto hao.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chama hicho, Zanini Athuman, wakati wa kukabidhi msaada huo wakishirikiana na Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO) nchini amesema katika kusherehekea siku hiyo wameiomba Serikali na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuridhia Mkataba wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) Namba 189, unaohusu kazi zenye heshima kwa wafanyakazi wa majumbani.

Amesema Wafanyakazi wa majumbani wana umuhimu wao mkubwa katika jamii na changamoto nyingi wanazokabiliana nazo, huku wakisisitiza kuwa nyumba za waajiri wao zinapaswa kutambuliwa rasmi kama Ofisi zao.

Athuman amesema wafanyakazi hao kwa muda mrefu wamekuwa wakinyanyasika kwa kubakwa,kupigwa,kutakiwa kimapenzi na wenye nyumba na wengine kutolipwa stahiki zao huku kukiwa hakuna wa kuwasema.

“Sisi tuna mchango mkubwa sana katika jamii na vile vile tunaongeza kipato katika nchi. Uwepo wetu huwezesha viongozi kama wabunge, mawaziri, watumishi wengine wa serikali, na akina mama wafanyabiashara kwenda kutekeleza majukumu yao huku wakijua kuwa nyumba zao na familia zao zimetunzwa na sisi ambao tunakuwa walimu,walinzi na pia wazazi katika nyumba zao,” asema.

Akizungumzia msaada waliokabidhi kwa watoto hao alisema wameguswa kwa kuwa asilimia kubwa ambao wamekuwa wakiwahudumia majumbani ni watoto na kina mama, hivyo wameona waonyeshe upendo huo kwao katika siku hii ya wafanyakazi majumbani.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa kuboresha ufanyaji kazi mahala pa kazi kwa wafanyakazi majumbani kutoka Shirika la Kazi la Kimataifa(ILO), Chiku Khamis, alisema majumbani ni sehemu ya kazi kwa wafanyakazi hao hivyo ni vema wakaheshimiwa na kuthaminiwa kama wafanyakazi wengine.

“Tunashukuru Chodawu kutualika kuwa pamoja nao katika siku ya leo, siku ya leo ni siku ambayo mkataba wa kitaifa 189 uliridhiea mjini Geneva na mkaya huu ulikuja baada ya kuona wafanyakazi wa majumbani ni wafanyakazi kama wengine lakini kuna haki na stahiki zao hawazipati.

“Mkataba huu uliundwa ili kuhakikisha kazi zenye staha kwaajili ya wafanyakazi wa majumbani ndio walezi na wameonesha umoja wao leo kuja hospitalini na kuleta vifaa kwaajili ya mama na watoto kuonesha kiasi gani wao ni walezi na wanajali familia zetu,” alisema.

Naye Msimamizi wa wodi ya watoto, Mary Machema, aliwashukuru Chodawu kwa msaada wao na kueleza utawasaidia katika kuwahudumia watoto hao ambao wengine wazazi wao hawana uwezo na wengine hawana wazazi kabisa.

Mary alisema wodi hiyo imekuwa ikipokea watoto wachanga wenye matatizo mbalimbali yakiwemo ya upumuaji, kuzaliwa na uzito mdogo au kupata maambukizi wakati na baada ya kuzaliwa.

spot_img

Latest articles

‘Energy drinks’ zitaangamiza taifa

KILA mwaka wa uchaguzi serikali ina kawaida ya kutoa bajeti inayogusa wananchi walio wengi,...

Rais Samia: Mwelekeo ni elimu ya ujuzi kwa vijana kumudu soko la ajira

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema...

Rais Samia: MEATU mtaendelea kupata miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo Nishati

📌Asema baada ya Vijiji vyote Meatu kupata umeme kasi inaelekea vitongojini 📌 Ataka umeme utumike...

GFA yaweka rekodi uundaji magari nchini, yakamilisha gari ya 4000

Na Mwandishi Wetu Kiwanda cha kwanza kutengeneza na kuunganisha magari Tanzania cha GF Vehicles Assemblers...

More like this

‘Energy drinks’ zitaangamiza taifa

KILA mwaka wa uchaguzi serikali ina kawaida ya kutoa bajeti inayogusa wananchi walio wengi,...

Rais Samia: Mwelekeo ni elimu ya ujuzi kwa vijana kumudu soko la ajira

Na Mwandishi Wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema...

Rais Samia: MEATU mtaendelea kupata miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo Nishati

📌Asema baada ya Vijiji vyote Meatu kupata umeme kasi inaelekea vitongojini 📌 Ataka umeme utumike...