Wizara ya Elimu yazindua kituo cha huduma kwa wateja

Na Mwandishi Wetu

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imezindua Kituo cha Huduma kwa wateja, kilichograimu takribani  Sh 100 milioni kwa lengo la kuanza kupokea ushauri,maoni na mawazo ya watu mbalimbali ili kuhakikisha  wizara hiyo inaendelea kuboresha sekta ya elimu.

Kituo hicho kimefadhiliwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya Uingereza kupitia ofisi yake ya Commonwealth na mradi wa shule bora

Akizungumza jijini Dodoma baada ya kuzindua Kituo hicho Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Omari Kipanga, amesema kuwa kupitia kituo hicho anaamini wataweza kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo zipo katika Wizara hiyo.

“Kupitia kituo hichi tutaenda kutatua changamoto pamoja na kwenda kufanya kazi kwa weledi lengo letu tunataka wizara yetu izidi kusonga mbele katika masuala ya elimu,”amesema Kipanga.

Aidha amesema kuwa  Serikali kupitia wizara hiyo  iliona ni muhimu kuwa na kituo hicho ili kuanza kupokea ushauri,maoni na mawazo ya watu mbalimbali ili kuhakikisha wanaendelea kuboresha elimu.

“Kipekee niwashukuru na kuipongeza serikali ya Uingereza kwa  kukiboresha kituo hiki kutoka Call Center hadi Contact Center na sisi tunaahidi tutatunza vifaa walivyowezeshwa,” ameeleza.

Hata hivyo amesema kuwa  wafanyakazi wa kituo hicho tayari wameshapata mafunzo na wana amini  watafanyakazi kwa weledi kuhakikisha wanawahudumia watanzania.

Awali Katibu Mkuu  wa Wizara hiyo Prof.  Carolyne Nombo,amesema kuwa kituo hicho wamekisubiri kwa muda wa miaka miwili na  sasa kimekamilika.

“Kupitia kituo hiki tunaenda kuwasiliana na wananchi katika maboresho ya elimu, Wizara  itaenda kutunza kituo hiki na kuhakikisha kwamba huduma ambazo zinatolewa zitakuwa bora na katika miaka ijayo,” amesema Prof.Nombo

Kwa upande wake Mwakilishi wa Ubalozi wa Uingreza Dk.John Lusingu,ametoa wito kwa watendaji wa wizara hiyo kutekeleza maoni ya wananchi.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...