Rais Mwinyi akaribisha   wawekezaji Wachina  kuendeleza tafiti za dawa   za asili

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka China kuwekeza nchini hususan kuendeleza sekta ya afya na tafiti za dawa za asili nchini.

Rais Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na timu ya wataalamu kutoka Chuo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha China waliofika Ikulu kuonana naye.

Aidha amesema Zanzibar imeendelea kuthamini mchango na misaada ya China kwa Zanzibar katika sekta tofauti za maendeleo na kijamii iliyodumu kwa muda mrefu tangu na baada ya Mapinduzi na kuendelea hadi sasa.

Halikadhalika, ameeleza kufarijika na misaada katika sekta ya sfya inayotolewa na timu za madaktari bingwa wanaokuja nchini kwa nyakati tofauti kutoa matibabu kwa Jamii, dawa na huduma katika Hospitali na vituo vya afya na mafunzo kwa watendaji wa sekta ya afya nchini.

Naye kiongozi wa ujumbe huo Naibu Mkurugenzi wa Chuo cha Utafiti wa Dawa za Asili cha China, Professa Song Li Jwan amesema ziara yao Zanzibar imelenga kuimarisha ushirikiano baina ya China na Zanzibar hususan katika maendeleo ya sekta ya afya na kuendeleza tafiti za dawa za asili baina ya pande hizo mbili.

Amebainisha kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa sera ya kitaifa ya China kwa nchi za Afrika ikiwa ni utekelezaji wa Malengo ya Mkutano wa Beijing wa mwaka 2024 uliojikita katika uimarishaji wa Sekta ya Afya.

spot_img

Latest articles

Timu ya Taifa kriketi ya wanawake kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia

Na Mwandishi Wetu Timu ya Taifa ya wanawake ya mchezo wa kriketi ya Tanzania inatarajiwa...

Ratiba ya Ligi Kuu msimu wa 2025/26 hadharani, Dabi ya Kariakoo Des 13

Na Winfrida Mtoi Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara(TPLB) leo  Agosti 29, 2025,  imetangaza ratiba...

Gari, Pikipiki, dhahabu, simu janja zaongeza msisimko katika mnada wa Piku

Na Mwandishi Wetu JUKWAA la kidigitali la PIKU linalojulikana kwa kuendesha minada ya kipekee...

TACTIC yaimarisha huduma za usafiri na usafirishaji Manispaa ya Sumbawanga

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Uendelezaji Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) unaelezwa kuimarisha huduma...

More like this