Raia wa Nchi 72 kuingia Tanzania bila Viza

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SERIKALI imeingia makubaliano na nchi mbalimbali ili kurahisisha utaratibu wa viza ambapo raia wa nchi 71 hawahitaji viza wanapoingia nchini.

Kwa sasa watalii kutoka mataifa mengi zaidi duniani wanaruhusiwa kupata visa wanapowasili (visa on arrival) kwenye viwanja vya ndege vya kimataifa kama Julius Nyerere (Dar es Salaam), Kilimanjaro na Zanzibar.

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Ualii, Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akijibu swali la Dkt. Pius Stephen Chaya aliyetaka kujua ni jitihada gani zimefanyika kurahisisha upatikanaji wa VISA kwa Watalii wenye uraia tofauti wanaokuja nchini kwa mwitikio wa Tanzania the Royal Tour.

Aidha Kitandula aliongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha utaratibu wa utoaji wa viza nchini ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Mathalan, Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imeanzisha mfumo wa maombi ya viza kwa njia ya mtandao (e-Visa) unaowawezesha watalii kuomba viza popote walipo duniani bila kulazimika kufika ubalozini.

“Halikadhalika, Serikali imeboresha Kanuni za Uhamiaji za mwaka 2023 (GN 428) ambapo kwa sasa watalii wanaotumia Visitors Pass wanaruhusiwa kutembelea Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kurejea Tanzania bila hitaji la kuomba upya pasi ya kuingia nchini,” alisema Kitandula.

Suala la visa lina uhusiano wa moja kwa moja na sekta ya utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii imeimarisha ushirikiano na Wizara ya Mambo ya Ndani, hususan Idara ya Uhamiaji, katika nyanja mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa takwimu za watalii na kuwa na mikakati ya pamoja ya kuvutia watalii na fursa za uwekezaji.

Hivi karibuni, Wizara kupitia Chuo cha Taifa cha Utalii imetoa mafunzo ya Huduma kwa Wateja na Ukarimu kwa Maafisa wa Jeshi la Uhamiaji ili kuboresha huduma zinazotolewa kwa wageni wanaoingia nchini, ikiwemo watalii.

spot_img

Latest articles

Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na...

Rais Mwinyi azindua Baraza la Wawakilishi, ataja mwelekeo wa Serikali atakayounda

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

More like this

Heche viongozi wengine Chadema waachiwa na Polisi kwa dhamana

Na Mwandishi Wetu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche na...

Rais Mwinyi azindua Baraza la Wawakilishi, ataja mwelekeo wa Serikali atakayounda

Na Mwandishi Wetu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali...