Bei ya Petroli, Dizeli zashuka

Na Mwandishi Wetu

BEI ya petroli, dizeli na mafuta ya taa kwa mwezi Juni 2025, imeendelea kuleta nafuu kwa watumiaji wa vyombo vya moto, nchini, ikilinganishwa na bei za mwezi Mei 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 4 Juni 2025, kwa mafuta yaliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imeshuka kwa shilingi 72.16, dizeli kwa shilingi 51.89 na mafuta ya taa shilingi 184.93.

Kwa Bandari ya Tanga, petroli imeshuka kwa shilingi 69.41 huku dizeli ikishuka kwa shilingi 50.1, Mtwara, petroli imeshuka kwa shilingi 71.65 na dizeli shilingi 51.37.

Aidha, ulinganifu wa bei za mafuta kwa miezi mitatu, Aprili, Mei na Juni 2025, mwenendo umeonesha kuendelea kushuka kwa bei maradufu kutoka shilingi 2905.34(Aprili) hadi 2,684.54(Juni) sawa na kupungua kwa shilingi 220.8 petroli iliyopokelewa bandari ya Dar es Salaam.

Tanga, petroli ilipungua kutoka shilingi 2904.93 hadi 2750.34 ikiwa ni tofauti ya shilingi 154.59 na kwa bandari ya Mtwara, kutoka shilingi 2811.36 hadi 2750.34 ikiwa imepungua kwa shilingi 154.59.

Kwa upande wa dizeli, kutoka Aprili hadi Juni 2025, bei zimepungua kwa shilingi 60.17 Dar es Salaam, 115.25 Tanga na 119.97 kwa Mtwara.

Bei za Juni 2025, zimeakisi kupungua kwa bei za mafuta katika soko la dunia kwa asilimia 0.9 ya kwa mafuta ya petroli, asilimia, 3.4 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 3.7 kwa mafuta ya taa mtawalia; hali iliyochagiza kupungua kwa bei kikomo za Juni 2025.

Vilevile, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umepungua kwa asilimia 0.63 huku gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es salaam zikiwa zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 4.34 kwa mafuta ya petroli, asilimia22.43 kwa mafuta ya dizeli na kupungua kwa asilimia 1.65.

Kwa upande wa Bandari ya Mtwara, gharama za uagizaji zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 51.55 kwa mafuta ya petroli na hakuna mabadiliko kwenye mafuta ya dizeli.

Ikumbukwe kuwa pia, viwango vipya vya kusafirisha bidhaa za mafuta vilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 5083 la tarehe 25 Aprili 2025 ndivyo vilivyotumika katika ukokotoaji wa bei kikomo za rejareja za bidhaa za petroli zilizoanza kutumika leo.

spot_img

Latest articles

Tanesco yashinda Tuzo ya uhifadhi wa Mazingira kupitia Mradi wa JNHPP

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa...

Dkt. Biteko aweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kituo kikubwa cha gesi Afrika Mashariki

📌 Tanga kuwa Kitovu cha Nishati nchini 📌 Dkt. Biteko Asisitiza Ajira Kwa Wazawa 📌Kampeni ya...

Dkt. Mpango awataka wadau wa Mazingira kuendeleza upandaji miti

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip...

Aliyekuwa Rais wa Zambia, Edgar Lungu afariki dunia

Na Mwandishi wetu Rais  wa  zamani  wa Zambia, Edgar Lungu, amefariki dunia  akiwa na umri wa miaka 65 baada...

More like this

Tanesco yashinda Tuzo ya uhifadhi wa Mazingira kupitia Mradi wa JNHPP

Na Mwandishi Wetu SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limekabidhiwa tuzo ya uhifadhi wa...

Dkt. Biteko aweka jiwe la Msingi ujenzi wa Kituo kikubwa cha gesi Afrika Mashariki

📌 Tanga kuwa Kitovu cha Nishati nchini 📌 Dkt. Biteko Asisitiza Ajira Kwa Wazawa 📌Kampeni ya...

Dkt. Mpango awataka wadau wa Mazingira kuendeleza upandaji miti

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip...