ASKARI JWTZ ASHIKILIWA NA POLISI KWA ULEVI

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro  limemkamata Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Daines Faustine (33) kwa tuhuma za kukutwa akiendesha gari akiwa amelewa kupita kiasi, hali iliyosababisha kushindwa kulidhibiti gari hilo na kugonga taa za barabarani katika eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro.

Kwa mujibu taarifa ya  Kamanda wa Polisi mkoani humo, Alex Mkama, tukio hilo limetokea Mei 17, 2025,  ambapo Faustine ambaye ni mkazi wa Morogoro, alikuwa akiendesha gari aina ya Nissan Juke alipokamatwa. Uchunguzi wa kitabibu umebaini alikuwa na kiwango cha pombe mwilini cha 305.9.

Amesema katika tukio lingine, dereva Bakari Omari (47), mkazi wa Kondoa mkoani Dodoma, amekamatwa akiendesha gari mali ya Kampuni ya Machame Investment  judoka Dar es Salaam kwenda Dodoma bila kuwa na leseni.

Kamanda Mkama amesema  uchunguzi umebaini kuwa dereva huyo alikuwa tayari amepigwa marufuku kuendesha magari tangu Mei 5, 2025, kufuatia mwenendo wake wa kuendesha mwendo hatarishi barabarani. Hata hivyo, alikaidi agizo hilo na kuendelea kuendesha gari kwa kificho hadi aliponaswa na vyombo vya usalama Mei 18, mwaka huu 2025.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linaendelea na operesheni maalum ya kudhibiti usalama katika barabara zote mkoani humo. Lengo kuu la operesheni hii ni  kulinda na kuokoa maisha ya watumiaji wote wa barabara pamoja  na vyombo vya moto kwa kuhakikisha sherry na kanuni  za usa lama barabarani  zinazingatiwa,” imesema taarifa hiyo.

spot_img

Latest articles

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

Serikali yawataka Wakurugenzi kuongeza thamani inayopimika katika uwekezaji wa hisa chache

Na Mwandishi wetu SERIKALI imewataka wakurugenzi wa bodi za kampuni ambazo ina umiliki wa...

Tanesco yazindua ndege nyuki (Drones) kuboresha miundombinu ya umeme nchini

📌Ni sehemu ya utekelezaji wa mikakati yake kuimarisha huduma kwa wateja kwa kutumia njia...

More like this