Shirika la Posta Tanzania lashiriki kongamano la eLearning Afrika, laja na huduma ya Swifpack

Na Tatu Mohamed

SHIRIKA la Posta Tanzania ni miongoni mwa washiriki katika kongamano la 18 la eLearning Afrika ambapo limetambulisha huduma ya ‘Swifpack’.

Swifpack inalenga kuchukua vifurushi na abiria kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urahisi kupitia simu janja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 09, 2025 katika banda lao lililopo katika kongamano hilo, Kaimu Meneja Mauzo Shirika la Posta Tanzania, Andrea Liundi amesema Swifpack inalenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi na kurahisisha usafirishaji wa mizigo au vifurushi.

“Kupitia maonesho haya ya eLearning Afrika, Shirika la Posta liko hapa kwaajili ya kutoa huduma kwa washiriki hasa wageni ambao wametoka nje kwaajili ya kushiriki hili kongamano.

“Pamoja na mambo mengine tuliyonayo, pia tumekuja na huduma ya Swifpack ambayo unadownload application kupitia simu janja. Kwamaana sasa hivi sio lazima uje ofisini kwetu kama unahitaji kutuma kifurushi bali unaingia Swifpack halafu unaita pikipiki au bajaji au gari,” amesema.

Ameongeza kuwa, katika kongamano hilo pia wanatoa huduma ya kusafirisha vifurushi kwenda ndani ya Tanzania na nje ya nchi.

“Lakini kikubwa zaidi hapa tupo kwaajili ya kutoa huduma ya kubadilisha fedha za kigeni. Tumeona kwamba wageni wakija hapa wanahitaji kubadilisha fedha na kupata za kitanzania kwaajili ya kufanya manunuzi yao ya ndani.

“Na tunashukuru muitikio ni mzuri tangu tumeanza juzi tumeweza kupata wageni wengi ambao wameenda kubadilisha fedha, pia Watanzania wameenda wanahitaji Dola. Na hiyo imetufanya tunatoa huduma hata nje ya muda wa kazi na hii ndo inaonesha jinsi gani kunauhitaji wa hii huduma,” amesema.

spot_img

Latest articles

Kapinga azindua Kituo Mama cha gesi asilia iliyoshindiliwa (CNG) DAR

📌 Ni cha Pili kwa ukubwa barani Afrika, Cha Kwanza kwa ukubwa EAC 📌 Kujaza...

Mapato yasiyo ya kodi yafikia asilimia 67, OMH yadhamiria kufikia lengo la mwaka

Na Mwandishi Wetu SERIKALI kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), imeendelea kuonesha mafanikio...

Dkt. Biteko: Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia kufikia asilimia 75 mwaka 2030

Na Mwandishi Wetu 📌 Dkt. Biteko akutana na Balozi wa Japan nchini 📌 Tanzania na...

Twange aanza kazi rasmi Tanesco

📌Aomba ushirikiano ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na umeme wa uhakika. 📌Aahidi Kuendeleza Mazuri yaliyofanyika...

More like this