Dkt Biteko: Serikali kuendelea kuwekeza katika sekta ya Afya

📌 Dkt. Biteko atambelea Hospitali ya Wilaya ya Meru

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeahidi kuendelea kuboresha huduma za Afya nchini katika ngazi zote ili kuboresha huduma za Afya kwa Watanzania.

Hayo yamesemwa Aprili, 25, 2025 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akiwa ziarani Mkoani Arusha ambapo amesema kuwa lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kusigeza huduma za afya kwa wananchi.

Akizungumza baada kutembelea Hospitali ya Wilaya ya Meru, iliyopo Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha, Dkt. Biteko amesema lengo la uwekezaji katika sekta ya afya ni kuboresha afya za Watanzania.

“Serikali inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea na uwekezaji mkubwa unaofanya kwa kujenga hospitali, vituo vya afya na zahanati katika maeneo mbalimbali nchini.

“Kama mnavyofahamu afya ndio mtaji wa wananchi na Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali mpya na kufanyia ukarabati zilizopo,” amesema Dkt. Biteko.

Amesistiza “Watu wote nilioongea nao hapa hospitalini wamesema hali ya utoaji huduma imeimarika na ni nzuri, nataka niwaambie Rais Samia katika uongozi wake ameapa kuboresha hali za maisha ya Watanzania.

“Hapo awali ilimlazimu mgonjwa kutoa makozi siku tatu mfululizo ili kumfanyia kipimo cha ugonjwa wa kifua kikuu, leo tuna mashine ya kisasa inayotumia saa mbili kupata majibu ya mgonjwa,”

Amesema ujenzi na maboresho yaliyofanyika hospitalini hapo imetumia raslimali za ndani (force account) na kazi imefanyika kwa ubora na kuzingatia thamani ya fedha.

Ameongeza kuwa katika kuelekea miaka 61 ya Muungano uwepo wa hospitali hiyo ni kiashiria cha kuwa nchi inapiga hatua kimaendeleo. Hivyo, wananchi hawana budi kuuenzi na kuutunza Muungano.

Aidha, amewataka wagonjwa kuwa wavumilivu wanapoenda kupata matibabu huku wakizingatia kuwa wahudumu wa afya wanafanya jitihada kubwa kuwapa huduma bora.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema kuwa wananchi wa eneo hilo wanafurahia huduma nzuri zinazotolewa na sasa idadi ya wagonjwa wanaohudumiwa ni 12,000 kutoka 3,000 ya awali.

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Meru, Daktari Elisante Fabiani amesema kuwa uboreshaji wa majengo katika hospitali hiyo umesaidia utoaji huduma na kuongeza idadi ya vipimo vya maabara kutoka 18 hadi 32.

“Tuna mashine ya kisasa ya kupimia vimelea vya kifua kikuu na ndani ya saa mbili pekee mgonjwa anapata majibu ya kifua kikuu na kuanza matibabu na ina uwezo wa kugundua dawa ya kutumia,” ameeleza Daktari Fabian.

Aidha, Dkt. Biteko ameendelea na ziara yake siku tano mkoani humo ambapo ametembelea Wilaya za Longido na Monduli ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

More like this

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...