Rais Samia afanya mazungumzo na Askofu Malasusa

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani ulioongozwa na Mkuu wa KKKT Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Aprili 11, 2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na viongozi hao wamejadili kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya afya ya akili.

Viongozi hao wa Kanisa wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano inaotoa kwa Kanisa hilo.

Aidha, kuhusu utoaji wa huduma kwa watoto wenye mahitaji maalum hususan wenye changamoto ya akili, Serikali imeahidi kushirikiana na Kanisa ili kujenga Kituo kikubwa zaidi ili watoto wengi waweze kupata huduma hiyo.

spot_img

Latest articles

Wanawake TRA Wapongezwa kwa Mchango wa Ukusanyaji Mapato

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, amewapongeza wanawake wa...

Mchungaji Kimaro: Miradi ya Familia Ndio Suluhisho la Ajira kwa Vijana

Na Mwandishi Wetu  MCHUNGAJI wa Kanisa la Kiinjiri Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama Dk....

Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani: TRA Yakabidhi Vifaa Tiba Vyenye Thamani ya Milioni 40

Na Tatu Mohamed KUELEKEA maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka Machi 8,...

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

More like this