GSM, EFTA zaungana kuwabeba wafanyabiashara wadogo na kati

Na Mwandishi Wetu

Taasisi ya kifedha ya EFTA na GSM zimeungana kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya kuwanufaisha wakulima na wafanyabiasha wadogo na kati kwa kuwawezesha kupata mikopo ya vitendea kazi kulingana na shughuli zao.

Mkataba huo umesainiwa leo Aprili 8, 2025 jijini Dar es Salaam ambapo ni muendelezo taasisi hiyo katika kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi nchini, kuwawezesha vifaa kama mashine, magari na vifaa vingine.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Makampuni ya GSM, Benson Mahenya amesema wameamua kushirikiana na EFTA kutokana na kutambua umuhimu wa shughuli za uzalishaji wanazozifanya pamoja na wateja wao.

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO)wa makampuni ya GSM, Benson Mahenya akibadilishana nyaraka na mkuu wa Masoko na Mauzo wa Kampuni ya EFTA nchini Clerius Asiel baada ya kusaini makubaliano ya kuwakopesha vitendea kazi ,Magari na mitambo wafanyabiashara wanaouza bidhaa za kampuni ya GSM bila dhamana jijini Dar es salaam .Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Uzalishaji wa Viwanda wa GSM Yassir Nassor.

Mahenya amesema kupitia mkataba huo, mawakala na wadau wanaosambaza bidhaa zao ambao wanakosa mikopo kwa vigezo vya kawaida wataweza kupata mikopo ya magari kutoka EFTA kupitia dhamana yao.

“Naamini kwa kufanya hivi tutagusa maisha ya kila mtu na kuongeza thamani ya biashara wa wadau wetu na kuongeza msaada,”

Ameeleza kuwa kutokana na shughuli nyingi wanazofanya ikiwamo usalishaji wa vinywaji, pia wamejikita zaidi katika kuimarisha usafirishaji wa matunda kama malighafi ili kuondoa uharibifu.

” Sisi tumeona ni vyema tukaimarisha usafirishaji wa matunda kwa kwenda eneo la uzalishaji ili yasiharibike na kupotea pia kumpa thamani mkulima,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mauzo na Masoko wa EFTA Tanzania, Clerius Asiel amesema kwa zaidi ya miaka 20 wamekuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiasha wadogo na kati nchini kwa kuwasidia kumiliki mashine na magari kwa mikopo nafuu bila dhamana.

Ameeleza kuwa mkataba huo na GSM umekuja baada ya kuwezesha upatikanaji wa magari zaidi ya 60 ya kusambaza bidhaa za kampuni hiyo.

” Hatua hii ni kielelezo cha maono yetu ya pamoja ya kukuza biashara endelevu, huku tukiwa na mchango wa moja kwa moja katika uundaji wa ajira na kuboresha kipato kwa wafanyabiashara wadogo.

” Kwa kuingia makubaliano haya GSM wanatupa nafasi ya kufanya biashara na wadau wao wote. Yaani leo hii kama ni mdau wa GSM ukihitaji kifaa chochote cha kusaidia katika biashara yako, taasisi ya EFTA itakupatia mkopo kuanzia wa mwaka mmoja hadi miaka mitatu”, amesema Asiel.

Amefafanua kuwa kwa mwaka jana pekee wameweza kutumia zaidi ya bilioni 48 kwa wakulima, wafanyabiashara na wajasiliamali.

Aidha ameeleza kuwa kwa kipindi cha miaka 20 wamefanikiwa kuwakopesha wajasiliamali 100,000 ambapo kiasi cha fedha walichotumia kinafikia sh 250 bilioni.

spot_img

Latest articles

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...

Kafulila: Hatuwezi kujenga uchumi wa nchi bila kushirikisha sekta binafsi

Na Tatu Mohamed, Mwanza MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma...

Mkoa wa Mwanza wawakaribisha wawekezaji, waanika fursa lukuki

Na Winfrida Mtoi, Mwanza MKOA wa Mwanza umeweka bayana utayari wake wa kutoa...

🔴🔴 Wananchi waguswa na miradi ya elimu inayotekelezwa na TAWA Liwale

📍Wakiri uhifadhi kuwa na manufaa Na Mwandishi wetu, Lindi MIRADI ya ujenzi wa madarasa mawili yenye...

More like this

Sekta binafsi zatakiwa kushiriki kikamilifu kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi

Na Tatu Mohamed, Mwanza  NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo...

Kafulila: Hatuwezi kujenga uchumi wa nchi bila kushirikisha sekta binafsi

Na Tatu Mohamed, Mwanza MKURUGENZI Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma...

Mkoa wa Mwanza wawakaribisha wawekezaji, waanika fursa lukuki

Na Winfrida Mtoi, Mwanza MKOA wa Mwanza umeweka bayana utayari wake wa kutoa...