EWURA, ERB kushirikiana kuboresha huduma za nishati

Na Mwandishi Wetu, Zambia

BODI ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Bodi ya Udhibiti wa Nishati Zambia (ERB) wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kimiundombinu ili kuboresha huduma za nishati katika nchi zao.

Wakati wa kikao baina ya Bodi hizo, zilizokutana Machi 24,2025 katika Ofisi za ERB Lusaka, imebainishwa kuwa hivi karibuni Taasisi hizo mbili zitasaini hati ya makubaliano kwaajili ya ushirikiano huo.Baadhi ya maeneo ambayo EWURA na ERB watashirikiana ni pamoja na kubadilishana taarifa za kitaalamu, kiuchumi na kimiundombinu, kujengea uwezo wataalamu, na kubadilishana uzoefu katika masuala ya kitaalamu.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya, amesema kuwa ushirikiano kati ya EWURA na ERB tayari umeleta mafanikio makubwa katika udhibiti wa sekta za petroli, gesi asilia, na umeme.

Ameongeza kuwa ushirikiano huo umechangia kuhakikisha uzingatiaji wa viwango vya usalama, mifumo ya kisheria, na ufanisi katika uendeshaji wa sekta hizo.

“Moja ya mafanikio makubwa ya ushirikiano wetu ni juhudi za pamoja katika ukaguzi wa bomba la mafuta la TAZAMA. Ukaguzi huu haujaimarisha tu usalama na ufanisi wa miundombinu hii muhimu, bali pia unadhihirisha dhamira yetu ya kuendeleza ubora wa udhibiti katika ukanda huu,” amesema Prof. Mwandosya.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya ERB Bw. James Banda amesema kuwa ushirikiano huo ni hatua muhimu kwa maendeleo ya sekta wanazosimamia na kusisitiza kuwa kusainiwa kwa hati ya makubaliano kutatoa msukumo zaidi katika kuboresha huduma za nishati na kuimarisha ufanisi wa kiutendaji.

spot_img

Latest articles

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-MAJALIWA

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya maboresho zaidi ya mazingira...

ALLY KAMWE  AKAMATWA NA POLISI AACHIWA  KWA DHAMANA

Na Mwandishi Wetu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema Jeshi la...

Bado watu wanapotea, yu wapi wa kuzuia hali hii?

ASKOFU wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk. Benson...

More like this

SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI-MAJALIWA

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kufanya maboresho zaidi ya mazingira...

ALLY KAMWE  AKAMATWA NA POLISI AACHIWA  KWA DHAMANA

Na Mwandishi Wetu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, SACP Richard Abwao amesema Jeshi la...