Dkt. Biteko: Ufundi Stadi umepewa kipaumbele na serikali

📌 Asisitiza kuwa, Rais Samia anajenga vyuo kila wilaya nchini

📌 Apongeza utoaji wa mafunzo na ujuzi kuendana na teknolojia ya kisasa

📌 Makundi maalumu kupewa kipaumbele

📌 Asema VETA itakuwa msingi kwa malezi ya watoto na Vijana

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamua kuwekeza kwenye ufundi ili Watanzania waweze kujikomboa katika uchumi.

Hayo yamebainishwa leo Machi 21, 2025 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA).

Dkt. Biteko amesema kuwa, Serikali imeweka msukumo mkubwa katika ufundi stadi ili Watanzania wapate elimu yenye viwango vikubwa na ujuzi wa kuweza kujikomboa katika nyanja za kiuchumi na kijamii.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anajenga VETA kila wilaya ili kuwapa ujuzi watanzania waweze kuajirika katika sekta zote,” amesisitiza Dkt. Biteko.

Aidha, ameipongeza VETA kwa maadhimisho hayo kwani ni hatua kubwa na kuwataka kuendelea kufanya kazi ili kuwajengea uwezo watanzania katika ujuzi mbalimbali.

“Kwa mara myingine nawapongeza VETA kwa kuendelea kutoa mafunzo na ujuzi kuendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuhakikisha kuwa ujuzi unatolewa kwa kuzingatia ubora na viwango vya kimataifa, ” amesema Dkt. Biteko.

Vile vile, amesisitiza elimu kutolewa kwa watu wenye mahitaji maalumu na wanaotoka kwenye mazingira magumu nchini yaweze kuongeza fursa kwa kila mtanzania kupata elimu ya ujuzi.

Naye, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema kwamba, Maadhimisho ya Miaka 30 ya VETA ni uhalisia kuwa Serikali imeipa kipaumbele VETA ili vijana wapate elimu ikiwemo kujenga vyuo vya ufundi katika maeneno mengi nchini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA, Anthony Kasore amesema kuwa, VETA imezingatia viwango na ubora wa mafunzo unazingatiwa ili vijana wanaohitimu waweze kumudu soko la ajira.

Aidha amemshukuru Rais Samia kwa usimamizi na uwezeshaji wake mkubwa katika mafunzo ya ufundi stadi nchini ili vijana waweze kupata maarifa na ujuzi ya kufanya shughuli za kiuchumi kwa tija.

spot_img

Latest articles

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

Rais Mwinyi: SMZ kuendelea kushirikiana na TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...

Tanzania yajumuishwa kwenye orodha ya Nchi zenye vikwazo vya kuingia Marekani

Na Mwandishi Wetu SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imethibitisha kuwa Serikali ya...

More like this

Katibu Mkuu Kiongozi awataka maofisa habari serikalini kujiimarisha kiutendaji kukabiliana na teknolojia

Na Winfrida Mtoi KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka amewataka Maofisa Habari wa Serikali...

Rais Mwinyi: SMZ kuendelea kushirikiana na TRA kuimarisha ukusanyaji wa mapato

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...