Bodi ya Wakurugenzi PURA yatua Songo Songo, yatoa neno utekelezaji miradi ya CSR

Na Mwandishi Wetu

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imefanya ziara maalum Songo Songo Mkoani Lindi kujionea hali ya miundombonu ya uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia, na utekelezaji wa miradi ya Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) unaofanywa na kampuni za utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia kisiwani humo.

Kupitia ziara hiyo, wajumbe wa Bodi walioshiriki akiwemo Mwenyekiti, Halfani Halfani walitembelea miundombinu ya kuzalisha na kuchakata gesi asilia inayoendeshwa na Kampuni ya PanAfrican Energy Tanzania Ltd (PAET) na mitambo ya kuchakata gesi asilia inayoendeshwa na GASCO ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akizungumza katika ziara hiyo, Halfani ameeleza kuwa kwa sasa kuna ongezeko la jitihada zinazowekwa na TPDC na PAET katika kutekeleza miradi ya CSR tofauti na hali ilivyokuwa awali. Katika hili, Halfani aliishukuru Serikali kwa kuhimiza suala la CSR kupitia ufuatiliaji thabiti na miongozo iliyoandaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015.

“Mimi ni mmoja wa watu ambao tulikuja Songo Songo enzi hizo. Tunafarijika kuona wamejenga shule ya msingi, shule ya sekondari na wamejenga bweni la wasichana, shule ya awali, na leo tumeona wamejenga kituo cha afya kikubwa tu, na walikuwa wakilipia ada wanafunzi wa kike waliokwenda kusoma Kilwa, tunafarijika kwamba miaka 20 baadae wanafunzi wa Songo Songo wanaweza kupata elimu hizi zote kama faida mojawapo ya kuwepo kwa mradi huu wa gesi asilia hapa” amesema Halfani.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PURA Mhandisi Charles Sangweni amesema ziara imelenga kuongeza uelewa kwa Wajumbe wa Bodi kwani kwa kufanya hivyo kutawawezesha kufahamu mambo kwa uhalisia wake na kuyatolea maamuzi.

“Sisi kama PURA, moja ya shughuli zetu ni kusimamia shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi nchini, na kusimamia uzalishaji, na ili kujenga ufahamu kwa watendaji pamoja na Wakurugenzi wa Bodi, huwa tunafanya ziara hizi mara kwa mara, ziara hii ni muhimu kwa sababu imehusisha Wajumbe wa Bodi lengo ni kuwawezesha kuona uhalisia wa shughuli zinazoendelea ambazo huwa wanazijadili na kuzitolea maamuzi na ushauri mara kwa mara” amesema Mhandisi Sangweni.

Akitoa neno katika ziara hiyo, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya PURA Mhandisi Hamdun Mansur amesema ziara hiyo imewafundisha mambo mengi ya uchakataji wa gesi asilia, na kuwataka PURA kuendelea kusimamia majukumu yao ipasavyo.

spot_img

Latest articles

Waziri Mkuu atoa sababu yakutotaja idadi vifo vilivyotokea Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema ni muhimu watanzania kutanguliza utu na...

Niffer arudishwa gerezani, 20 kesi ya uhaini waachiwa huru

Na Mwandishi Wetu Watuhumiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini wameachiwa...

Dk.Mwigulu aagiza Kanisa Gwajima lifunguliwe

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na...

Ndejembi asisitiza ushirikiano kwa viongozi katika utekelezaji wa miradi yenye kipaumbele kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi (Mb), ametoa wito kwa viongozi na...

More like this

Waziri Mkuu atoa sababu yakutotaja idadi vifo vilivyotokea Oktoba 29

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amesema ni muhimu watanzania kutanguliza utu na...

Niffer arudishwa gerezani, 20 kesi ya uhaini waachiwa huru

Na Mwandishi Wetu Watuhumiwa 20 kati ya 22 waliokuwa wanashtakiwa kwa makosa ya uhaini wameachiwa...

Dk.Mwigulu aagiza Kanisa Gwajima lifunguliwe

Na Mwandishi Wetu Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba ameagiza kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na...