ALAT yawataka Madiwani kuwaelezea wananchi yaliyofanywa na Dkt. Samia

Na Mwandishi Wetu

MADIWANI nchini wametakiwa kuanza kufanya mikutano ya hadhara katika maeneo yao ili kuwaelezea wananchi mambo mbalimbali yaliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Taifa, Murshid Ngeze katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema mikutano hiyo ya hadhara ifanyike katika maeneo mbalimbali ambapo itasaidia wananchi kuyafahamu mazuri yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita.

“Tunafahamu yapo mengi ambayo yanayoelezeka na kuonekana kwa mfano ujenzi wa madarasa, vituo vya afya, barabara na mengine mengi, lakini yapo ambayo hayaonekani mfano ajira.

“Hivyo nitoe wito kwa Madiwani wenzangu katika maeneo yenu fanyeni mikutano ya hadhara kuwaelezea wananchi mambo haya mazuri yaliyofanywa na Rais wetu Dkt. Samia,” amesema.

Akitolea mfano amesema Dkt. Samia alipoingia madarakani mwaka 2021 wa kulikuwa na uhaba wa watendaji wa vijiji na mitaa.

“Mfano Halmshauri ya Bukoba sisi tuna vijiji 94 wakati Rais Dkt Samia anaingia madarakani, vijiji 40 ndo vilikuwa na watendaji lakini leo hakuna Kijiji chochote ambacho hakina Mtendaji wa Kijiji.

“Kwa upande wa eneo la ajira, kulikuwa na upungufu wa walimu na watumishi wa sekta ya Afya lakini Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia imeweza kutia ajira nyingi katika Kanda hizi,” amesema.

Aidha ametolea mfano katika zao la kahawa amesema tangu Rais Dkt. Samia aingie madarakani kilo moja ilikua ikiuzwa 2100 hadi 2500 lakini kwa sasa imefikia 5500 hadi 6000.

“Haya ndio mambo ameagiza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan twende tukayaseme kwa wananchi ili waweze kuelewa na kujua kwamba mama amefanya kazi,” ameisitiza Ngeze.

Aidha amesema ALAT mejiwekea mikakati mbalimbali ikiwemo kujenga jengo la kitega uchumi jijini Dodoma na kuongeza Mafunzo kwa watendaji wa Serikali za Mitaa.

“Pia tuna mpango wa kutafuta wataalumu bobezi wa masuala ya uchumi ili kuibua vyanzo vya mapato kwa Halmashauri ambazo Mapato yake yako chini,” ameongeza.

Vilevile amesema ALAT wanatamani kuwe na wiki ya serikali za mitaa ili waweze kuonyesha shughuli mbalimbali zinazofanywa pamoja na kutangaza mafanikio yake.

spot_img

Latest articles

MC Pilipili afariki dunia

Na Mwandishi Wetu Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' amefariki dunia leo,...

Watahiniwa 595,816 kuanza Mtihani wa Kidato cha Nne kesho

Na Tatu Mohamed JUMLA ya watahiniwa 595,816 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025...

Tume kuundwa kuchunguza vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu

Na Mwandishi Wetu  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza...

Mkakati wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya kupikia: Dira ya Mafanikio ya Taifa

Na Mwandishi Wetu IMEELEZWA kuwa Mkakati wa Mawasiliano wa Nishati Safi ya Kupikia ni...

More like this

MC Pilipili afariki dunia

Na Mwandishi Wetu Mchekeshaji na mshereheshaji maarufu nchini, Emmanuel Mathias 'MC Pilipili' amefariki dunia leo,...

Watahiniwa 595,816 kuanza Mtihani wa Kidato cha Nne kesho

Na Tatu Mohamed JUMLA ya watahiniwa 595,816 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne 2025...

Tume kuundwa kuchunguza vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka huu

Na Mwandishi Wetu  RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametangaza...