TUJIEPUSHE KUIGA TABIA ZA KIGENI ZISIZOKUWA NA MAADILI KWA TAIFA-MAJALIWA

Na Mwandishi Wetu

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema jamii inahitaji kufundishwa, kutambua na kuenzi mila za Kitanzania, pamoja na kujiepusha na vishawishi vya kuiga tabia za kigeni ambazo hazina manufaa kwa ustawi wa Taifa.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Machi 19, 2025 katika Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu wa Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki Bukoba Askofu Method Kilaini.

“Sote tumekua tukishuhudia ongezeko la vitendo vya ukosefu wa maadili katika jamii. Vitendo hivi vinatokana na malezi hafifu lakini pia watu kuiga mila na desturi kutoka mataifa mengine ambazo haziendani na tamaduni na maadili yetu ya Kitanzania,” amesema.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Askofu Msaidizi Mstaafu, Method Kilaini katika Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu Method Kilaini kwenye Kanisa Kuu la Jimbo Katoliki la Bukoba, Machi 19, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu amesema hali hiyo imeathiri mwenendo wa jamii, hususan kwa vijana ambapo wanashuhudia mabadiliko katika misingi ya familia, jamii, na Taifa kwa ujumla. “Nitumie fursa hii kuliomba Kanisa kuendelea kuwa nguzo ya maadili bora, kwa kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii,”

Amesema Kanisa lina nafasi ya pekee katika kuhakikisha Taifa linarudisha maadili ya kweli ya Kitanzania yanayofundisha kuheshimu utu, haki na amani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo (kulia) na Askofu Msaidizi Mstaafu Method Kilain katika Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wa Askofu Msaidizi Mstaafu Kilaini iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu  la Jimbo Katoliki la Bukoba, Machi 19, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

“Serikali, tunatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika hili na tutashirikiana nalo ili kuleta mabadiliko chanya kwa kizazi cha sasa na kijacho,” amesema.

Amesema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa madhebu ya dini ikiwemo Kanisa Katoliki katika kuboresha ustawi wa jamii yetu, hivyo amewaomba viongozi wa dini nchini waendelee kuwa nguzo ya maadili bora, kwa kutoa mwongozo wa kiroho na kijamii.

Akizungumza kuhusu Askofu Kilaini, amesema ni kielelezo cha ujasiri, imani thabiti, na huduma ya kujitolea kwa Kanisa na jamii ya Watanzania, ameonesha nguvu ya uvumilivu, akiwa na michango mikubwa katika maisha ya kanisa.

spot_img

Latest articles

Wakurugenzi Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa kwa siku tano

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) kwa kushirikiana na Taasisi ya...

Mkurugenzi Mkuu NIRC atoa pole kwa waandishi wa habari waliopata ajali Iringa

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa,...

Baraza la wafanyakazi Siri ya utendaji bora

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Wafanyakazi la Sita la TMDA limefanyika kwa ufanisi tarehe...

Baraza la sita la wafanyakazi lachagiza mafanikio ya TMDA

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, ametoa pongezi kwa wajumbe...

More like this

Wakurugenzi Ofisi ya Msajili wa Hazina wapigwa msasa kwa siku tano

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) kwa kushirikiana na Taasisi ya...

Mkurugenzi Mkuu NIRC atoa pole kwa waandishi wa habari waliopata ajali Iringa

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC), Raymond Mndolwa,...

Baraza la wafanyakazi Siri ya utendaji bora

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Wafanyakazi la Sita la TMDA limefanyika kwa ufanisi tarehe...