DC Kibaha afungua Baraza Kuu la Wafanyakazi DAWASA

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Wilaya ya Kibaha, Nickson Simon amefungua kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Akifungua kikao hicho katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Wilayani Kibaha, Nickson amewapongeza wajumbe wa baraza hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya inayopelekea kutoa huduma bora kwa wananchi.

Nickson amesema uhalali wa Serikali kuendelea kuwepo ni Wananchi kupata huduma za msingi, hivyo DAWASA wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya Majisafi na Majitaka ili serikali iendelee kuwepo.

Amesema maji yanaweza kuleta amani au yanaweza kuleta machafuko, hivyo maji ni muhimu, na wanachotaka wananchi wakiomba kuunganishiwa maji, waunganishiwe kwa haraka na maji yatoke kwenye bomba.

Amesema DAWASA imeiheshimisha sana Mkoa wa Pwani kwani wawekezaji wanapokuja kutaka kuwekeza tunawaambia huduma ya maji ipo ya kutosha.

“Wawekezaji wakija Pwani sisi tunawaambia tuna uhakika wa maji na hiyo inaongeza uwekezaji katika sekta ya viwanda katika mkoa wetu, sisi kufanya vizuri Mkoa wa Pwani kunatokana na uwepo wa maji ya kutosha kutoka DAWASA,” amesema Nickson.

Mkuu huyo wa Wilaya ameitaka DAWASA kuongeza kasi na juhudi katika kutoa huduma kwa wananchi ili kufikia malengo yao na kuhakikisha wananachi wanapata huduma bora wakati wote.

“Nawaomba DAWASA muongeze speed katika kutoa huduma, kuhakikisha mnadhibiti upotevu wa maji. Wananchi wa wilaya yangu, wao wanafurahia huduma za DAWASA hivyo nawapongeza sana,” amesema.

spot_img

Latest articles

Ndejembi: Ufanisi wa Tanesco katika utekelezaji na Usimamizi wa miradi umeleta mfumo madhubuti wa Nishati

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi, amesema kuwa Shirika la Umeme...

Maboresho ya mitambo ya kufua umeme Mtera yaimarisha uzalishaji umeme

Na Mwandishi Wetu, Mtera NAIBU Waziri wa Nishati, Salome Makamba, Novemba 26, 2025, alitembelea na...

Ndejembi: Tanzania sasa ina umeme wa kutosha

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amesema Tanzania kwa sasa ina umeme...

Jeshi la Polisi lachunguza  taarifa ya OCD  Chunya

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi limesema limeona na linafanyia uchunguzi taarifa inayosambaa kwenye mitandao...

More like this