Rais Samia: Ujenzi Kituo cha kupoza umeme Handeni kuimarisha upatikanaji umeme

📌 Kituo kugharimu shilingi bilioni 50

📌 Zaidi ya Shillingi billioni 98 kutekeleza mradi wa gridi imara Kilindi

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Handeni mkoani Tanga utakapokamilika utaboresha upatikanaji wa umeme katika Wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na maeneo jirani.

Rais Samia ameyasema hayo leo Februari 25, 2025 katika ziara yake mkoani Tanga wakati akizungumza na wananchi wa Handeni mara baada ya kuzindua Shule ya Wasichana ya Kilindi na Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.

“Tatizo la umeme hapa Handeni Serikali inalifahamu, imeanza kuchukua hatua kwa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kitakachogharimu takribani shilingi bilioni 50 za kitanzania ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme,” amesema Rais Samia.

Ameeleza kuwa, upatikanaji wa umeme wa uhakika Handeni utasaidia ukuaji wa uchumi pamoja na kuyainua madini ya kinywe ambayo yanapatikana Wilaya ya Kilindi na yanahitaji umeme wa kutosha.

Awali, Mbunge wa Kilindi, Omari Kigua aliishukuru Serikali kwa niaba ya wananchi kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 98 kwa ajili ya kutekeleza mradi ya gridi imara utakao husisha ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkata kupitia Handeni hadi Kilindi.

Kigua ameeleza kuwa Wilaya ya Kilindi ina Vijiji 102 ambavyo vyote vimefikiwa na umeme na sasa kazi inayoendelea ni ya kufikisha umeme kwenye Vitongoji.

spot_img

Latest articles

Mavazi ya kitamaduni kivutio kingine AFCON 2025

Na Winfrida Mtoi SHAMRASHAMRA kuelekea Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2025), zimezidi kupamba moto, hasa baada...

Livembe: Mchakato wa Uchaguzi ulikuwa wa haki na halali

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT), Hamis Livembe, amesema mchakato wa...

Sekta ya Viwanda na Biashara yazidi kutoa fursa kwa vijana

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga amesema sekta ya viwanda...

Polisi yachunguza tukio la kuchoma moto magari msibani

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro limesema linachunguza tukio la kuchoma moto na...

More like this