RAIS SAMIA: NAMRUDISHA MWANANGU JANUARI KWA MAMA, NILIMPIGA KOFI

Na Mwandishi Wetu

Rais Samia Suluhu Hassan amesema  anamrudisha Januari Makamba kwa mama kwani alimpiga kofi na kumfichia chakula  kama ilivyo desturi ya kina mama pindi mtoto anapomkera.

Rais Samia amezungumza hayo  leo Februari 24,2025 wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Lushoto mkoani, Tanga.

“Nataka nimuite mwanangu Januari hapa aje huku,arudi kwa mama, Sisi wamama mnatujua, ukimkera mama anakupiga kikofi, anakufichia chakula. Sasa mwanangu nilimpiga kikofi  na kumfichia chakula, lakini leo namrudisha kwa mama. Haya mwanangu njoo,” amesema Rais Samia huku akimkumbatia Makamba.

Katika hatua nyingine Rais Samia amezindua jengo la Halmashauri ya Bumbuli, wilayani humo na kusema kuwa madhumuni ya jengo hilo ni kusogeza huduma karibu ambapo na wananchi ambapo huduma zote zitakuwa zinapatikana humo.

spot_img

Latest articles

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...

CAF yaipiga faini Simba, kucheza bila mashabiki

Na Mwandishi Wetu Klabu ya Simba imepigwa faini ya Dola za Marekani 50,000 (...

More like this

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...