Kamati ya PIC yaona tija uwekezaji kiwanda cha uzalishaji bidhaa za ngozi

Na Mwandishi Wetu

KAMATI ya Bunge ya Uwekezaji na mitaji ya Umma (PIC) imepongeza serikali ya Awamu ya sita chini Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uwekezaji wenye tija na manufaa kwa maendeleo ya nchi katika kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za ngozi Kilimanjaro International Leather Industries Co Ltd.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda hicho mwenyekiti wa kamati hiyo, Agustine Holle amesema kuwa kutokana na uwekezaji wenye tija waliouona utaiwezesha serikali kuongeza mapato.

Amesema kiwanda hicho kitaunufaisha mkoa wa Kilimanjaro pamoja na mikoa ya jirani kwa kuboresha mfumo wa maisha na kuongeza kipato kwa wakazi hao.

Amebainisha kuwa wameridhika na uendeshaji wa Kiwanda hicho ambapo kitakapokamilika kwa asilimia 100 kinakwenda kutoa ajira 3,000 kwa ajira za moja kwa moja na ajira nyingine zisizo za moja kwa moja ni 4,000.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Ridhiwani Kikwete ameihakikishia kamati hiyo kuwa ataendelea kusimamia maono ya Dkt. Samia kwa kuufanya uwekezaji huo wenye tija unakuwa endelevu kwa manufaa ya watanzania na nchi.

spot_img

Latest articles

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...

SGR yapata ajali, TRC yataja chanzo

Na Mwandishi Wetu Treni ya Mwendokasi (SGR) imeacha njia yake na kupata ajali katika eneo...

More like this

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...