TMA:JUA LA UTOSI LIMESOGEA

Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema ongezeko la joto katika baadhi ya maeneo nchini limesababishwa na kusogea kwa jua la utosi sambamba na upungufu wa mvua.

Kwa mujibu wa tarifa ya Mamlaka hiyo, kwa kawaida vipindi vya jua la utosi nchini hufikia tamati mwishoni mwa mwezi Novemba wakati jua la utosi likiwa linaelekea kusini (Tropiki ya Kaprikoni) na hali hiyo hujirudia tena mwezi Februari wakati jua la utosi likiwa linaelekea kaskazini (Tropiki ya Kansa).

TMA imeeleza kuwa jua la utosi huambatana na hali ya ongezeko la joto kwa sababu uso wa dunia katika eneo tajwa huwa karibu zaidi na jua kuliko maeneo mengine ambapo katika kipindi cha Februari, 2025 hali ya ongezeko la joto imeendelea kujitokeza katika baadhi ya maeneo ambapo hadi kufikia tarehe 11 Februari, 2025 kituo cha hali ya hewa cha Mlingano (Tanga) kiliripoti kiwango cha juu zaidi cha nyuzi joto 36.0°C tarehe 05 Februari ikiwa ni ongezeko la nyuzi joto 2.1°C ikilinganishwa na wastani wa muda mrefu kwa mwezi Februari.

Kituo cha hali ya hewa kilichopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kiliripoti kiwango cha juu cha nyuzi joto 35.0°C mnamo tarehe 10 Februari, 2025 (ongezeko la nyuzi joto 2.2°C). Kituo cha Tanga kiliripoti nyuzi joto 35.1°C mnamo tarehe 10 Februari (ongezeko la nyuzi joto 2.3°C), Kibaha nyuzi joto 35.8 °C mnamo tarehe 10 Februari (ongezeko la nyuzi joto 3.0°C), na Kilimanjaro nyuzi joto 34.3°C mnamo tarehe 09 Februari, 2025 (ongezeko la nyuzi joto 0.6°C).

Aidha, imesema ongezeko la unyevu angani (Relative humidity) katika kipindi hiki linalosababishwa na mvuke wa bahari hususan katika maeneo ya ukanda wa pwani na maeneo jirani, pia limechangia mwili wa Binadamu kuhisi joto zaidi ya viwango vinavyoripotiwa ambapo vipindi vya ongezeko la joto vinatarajiwa kuendelea kujitokeza katika mwezi huu wa Februari, 2025 hususan katika maeneo ambayo msimu wa mvua za vuli umeisha.

spot_img

Latest articles

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

More like this

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...