Mkandarasi anayejenga Barabara za Tactic Morogoro atakiwa kukamilisha kazi ndani ya miezi mitatu

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila amemtaka Mkandarasi M/s Jiangxi GEO Engineering Group anayejenga barabara ya Kihonda – VETA yenye urefu wa Km 12.85 kwa kiwango cha lami Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa ubora unaotakiwa ndani ya miezi mitatu hadi kufikia mwezi Mei 2025.

Mhandisi Mativila ametoa agizo hilo kwa mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wa mradi huo katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo unaotekelezwa kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) chini ya mkopo nafuu toka Benki ya Dunia.

“Nimekuja kutembelea moja ya miradi mikubwa ambayo serikali ya awamu ya sita inatekeleza kwa ajili ya kuleta maendeleo na ushindani katika miji 45 ya Tanzania iliyochanguliwa iwe na ushindani wa kuwa na miundombinu bora ikiwemo ya barabara kwa kiwango cha lami inayowezesha kukua kwa uchumi’’, amesema.

Amefafanua kuwa, kati ya miji hiyo ni pamoja na Manispaa ya Morogoro ambayo inanufaika na utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambapo kwa mkoa huo mradi unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 19.6.

“Mradi huu umechelewa na upo nyuma kwa asilimia 18 na kwamba umetekelezwa kwa asilimia 82 tu na kuna sababu kadhaa ambazo zimeelezwa, baada ya kuweka mambo sawa tunataka mradi huu ukamilike ndani ya muda wa miezi mitatu endapo kukiwa na mvua kubwa basi mradi uwe umekamilika Agosti, mwaka huu“, amesema.

Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Mohamed Muanda amesema ujenzi wa mradi huo ulianza Oktoba 23, 2024 na kutakiwa kukamilika Februari 2025 ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa mifereji mikubwa ya maji ya mvua kuelekea mto Kikundi yenye urefu wa jumla ya Km 4.4, ujenzi wa ofisi ya Mhandisi Mshauri na ofisi ya wasimamizi wa miradi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mhandisi Mshauri kutoka nchini pamoja na Mhandisi Mshauri kutoka Ethiopia (JV Core consultancy), Dargie Dilbedi amemhakikishia Naibu Katibu kwamba kazi hiyo ipo katika hatua ya mwisho na kwamba anatumaini ndani ya miezi mitatu ya nyongeza itakamilika

spot_img

Latest articles

Yanga bingwa Mapinduzi Cup 2026

Na Mwandishi Wetu YANGA imetwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi ikiifunga Azam FC kwa mikwaju...

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...

‘Guardians of the Peak’ kuinua utangazaji utalii wa Kilimanjaro kupitia filamu

Na Mwandishi Wetu MRADI wa Guardians of the Peak, unaoingia msimu wake wa pili,...

More like this

Yanga bingwa Mapinduzi Cup 2026

Na Mwandishi Wetu YANGA imetwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi ikiifunga Azam FC kwa mikwaju...

Yacouba atambulishwa Mbeya City

Na Mwandishi Wetu NYOTA wa zamani wa Yanga, raia wa Burkina Faso, Yacouba Songne, ametambulishwa ...

Waziri Ndejembi: Tanzania ina fursa kubwa ya kuendeleza nishati ya Jotoardhi

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema kutokana na uwepo wa vyanzo...