Kapinga: Kituo cha kupoza umeme cha Uhuru wilayani Urambo kimekamilika

📌 Kinalenga kuboresha hali ya upatikanaji umeme Urambo na maeneo mengine

NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema ujenzi wa kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Uhuru kilichopo Wilaya ya Urambo mkoani Tabora umekamilika.

Kapinga ameyasema hayo leo Februari 07 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta aliyetaka kufahamu Serikali itakamilisha lini kituo hicho cha kupoza umeme na lini kitaanza kufanya kazi.

“Mhe. Spika ujenzi wa kituo cha kupoza umeme umeshakamilika, hivi sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme, ikikamilika kituo hicho kitaanza kufanya kazi,” amesema Kapinga.

Akijibu swali la Mbunge wa Nanyumbu, Ally Mhata aliyetaka kufahamu lini Serikali itashusha bei ya kuunganisha umeme katika Kata za Mangaka na Kilimanihewa kama maombi yalivyowasilishwa Wizarani, Kapinga amesema kutokana na hali halisi ilivyo nchini, kuna maeneo ya vijiji na Vijiji Miji ambapo maeneo ya vijiji yanaunganishwa na umeme kwa gharama ya shilingi 27,000.

Ameongeza kuwa, maeneo yenye sura ya Vijiji-Miji yanaunganishwa kwa gharama ya shilingi 320,960 hivyo kwa maeneo ya Kata ya Mangaka na Kilimahewa yenye sura ya Vijiji Miji yana unganishwa umeme kwa gharama ya shilingi 320,960.

Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho ya gharama kutokana na tathmini iliyofanyika.

Kuhusu Vitongoji 105 ambavyo havijapata umeme Wilaya ya Nanyumbu, Kapinga amesema hivi sasa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya kupeleka umeme kwenye Vitongoji ikiwemo Vitongoji 15 kwa Mbunge na kwa mwaka ujao wa fedha vitaongezwa Vitongoji vingine 38 ili kupunguza idadi ya vitongoji hivyo 105.

spot_img

Latest articles

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...

Ofisi ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ya Sabasaba kutangaza huduma

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili Hazina yazitaka taasisi za umma kutumia maonesho ...

More like this

Neema Mchau ajitosa kugombea Udiwani Viti Maalum Ilala

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Kata ya Gongolamboto Neema Mchau amechukua fomu...

Amanzi na Babu Tale uso kwa uso Jimboni

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Tawi la Chuo...

VETA Pwani yabuni Mita ya Maji ya Kisasa, kutatua migogoro kwa wapangaji

Na Tatu Mohamed KATIKA hatua ya kuleta mageuzi katika usimamizi wa matumizi ya maji...