Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ashiriki ibada ya kumuaga mama mzazi wa Waziri Mkenda

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango leo Februari 06, 2025, wameungana na viongozi na wananchi mbalimbali katika Ibada ya kumuaga marehemu Sekunda Massawe ambaye ni Mama mzazi wa Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Ibada hiyo imefanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Pius X – Tarakea mkoani Kilimanjaro.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Mpango amesema Serikali, inashukuru kwa maisha ya mama Sekunda aliyemzaa na kumlea Prof. Mkenda, ambaye amekuwa Mtendaji na Kiongozi mahiri katika utumishi wa umma, tangu alipokuwa anafundisha Chuo Kikuu cha Dar es salaam na katika nafasi mbalimbali alizoshika Serikalini.

Amesema Taifa linaendelea kufaidi matunda ya malezi bora na uchapakazi, ambayo mama Sekunda aliwapatia watoto wake.

Ametoa rai kwa wazazi na walezi kufanya kila jitihada kusomesha watoto, kuwafundisha maadili mema, kushika dini yao kiadilifu, na kufanya kazi kwa bidii kwa faida yao wenyewe, familia na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa, kila mmoja anapaswa kujitahidi kuishi vema na binadamu wenzake na kufanya kazi kwa bidii katika nafasi mbalimbali ili kutoa mchango mzuri kwa familia na Taifa, na kuacha historia nzuri na mifano bora ya kuigwa na jamii. Ameongeza kwamba ni muhimu kujiandaa kumrudia Muumba maana hakuna ajuaye siku wala saa.

Ibada ya kumuaga marehemu Sekunda Massawe imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi Mhashamu Ludovick Minde na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wabunge, Viongozi wa Taasisi mbalimbali, Viongozi wa Dini pamoja na wananchi mbalimbali.

spot_img

Latest articles

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

Wanafunzi watatu wafariki dunia baada ya kupigwa na radi Dar

Na Mwandishi wetu WANAFUNZI watatu wa Shule ya Msingi Msongola iliyopo eneo la Msongola,...

More like this