Bei ya Petroli, dizeli zapanda

Na Mwandishi Wetu, Dodoma 

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji – EWURA, imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli nchini ambazo zimeanza kutumika kuanzia leo Februari 05, 2025.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo Februari 5, 2025, bei ya petroli kwa rejareja katika Jiji la Dar es Salaam imeongezeka kwa asilimia 0.957, dizeli kwa asilimia 2.18 na mafuta ya taa kwa asilimia 1.25.

Hii ikiwa na maana kuwa sasa wanunuzi wa mafuta kwa bei ya rejareja katika Jiji la Dar es Salaam watanunua lita moja kwa Sh. 2,820 kwa petroli, dizeli Sh. 2,703 na mafuta ya taa kwa Sh. 2,710.

Bei hizo ni kutoka Sh. 2,793 kwa bei ya petroli ndani ya jiji la Dar es Salaam kwa Januari mwaka huu, dizeli Sh. 2,644 na mafuta ya taa kwa Sh. 2,676.

spot_img

Latest articles

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...

Rais Samia: Hakuna mtoto atafika darasa la tatu bila kujua kusoma, kuandika na kuhesabu

Na Tatu Mohamed RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

More like this

CRDB yajipanga kuwezesha wabunifu Kibiashara

Na Mwandishi Wetu  BENKI ya CRDB imesema ipo tayari kuunga mkono tasnia ya ubunifu nchini...

MAB yateta na wadhibiti Mutukula OSBP

Na Mwandishi Wetu MWENYEKITI Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi...