Waziri Chana azitaka Halmashauri zote nchini kulinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi, Dkt. Pindi Chana amezielekeza Halmashauri zote nchini kuchukua jukumu la kulinda wananchi dhidi ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.

Ameyasema hayo leo Februari 04, 2025 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu swali la Mhandisi Ezra John Chiwelesa aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuondoa adha ya uvamizi wa tembo katika Kijiji cha Nyabugombe Kata ya Nyakahura – Biharamulo.

“Katika bajeti za Halmashauri asilimia 10 za bajeti za Halmashauri, mapato ya ndani na kuna maeneo Wizara ya Maliasili na Utalii inarudisha fedha za Wildlife Management Areas asilimia 25, fedha hizi zinatakiwa zitumike kwa shughuli rafiki za uhifadhi kulinda wananchi wasiumizwe,” amesisitiza Chana.

Amesema kuwa ajenda ya kulinda wananchi dhidi ya changamoto mbalimbali ikiwemo za wanyamapori wakali na waharibifu ni ajenda ya Halmashauri husika na kusisitiza kwamba halmashauri zina uwezo wa kununua ndege nyuki “drones”, kusomesha vijana kozi za uhifadhi ili wawe Askari wa Vijiji wajue namna ya kulinda wananchi.

Awali akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kukabiliana na adha ya wanyamapori wakali na waharibifu wakiwemo tembo katika maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa Burigi – Chato.

“Mikakati inayotekelezwa ni pamoja na: kuendelea kushirikiana na Wananchi kudhibiti tembo kwa wakati ambapo jumla ya Askari sita (6) wa uhifadhi kwa kushirikiana na mgambo sita (6) waliopewa mafunzo kuhusu tabia za wanyamapori wanatumika kufukuza tembo kupitia kituo cha Nyungwe kilichopo Kijiji cha Nyabugombe, Kata ya Nyakahura” amesema Kitandula.

Kijiji cha Nyabugombe kilichopo katika Kata ya Nyakahura, ni miongoni mwa vijiji 38 vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa Burigi-Chato. Kwa kipindi cha miezi sita Julai – Disemba, 2024 Jumla ya matukio 16 ya tembo yaliripotiwa na kudhibitiwa katika kijiji cha Nyabugombe kilichopo Kata ya Nyakahura, Wilaya ya Biharamulo.

spot_img

Latest articles

Mkurugenzi Mkuu Dawasa Mtaa kwa Mtaa kukagua huduma za maji

Na Mwandishi Wetu AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira...

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

More like this

Mkurugenzi Mkuu Dawasa Mtaa kwa Mtaa kukagua huduma za maji

Na Mwandishi Wetu AFISA Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira...

Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja...

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...